Wataalam 48 wa Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma wameanza mafunzo ya siku tano ya mfumo mpya wa ununuzi wa umma (NeST) yanayofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga.
Wakufunzi wa mafunzo hayo wanatoka Sekretarieti ya MKoa wa Ruvuma ambao siku chache zilizopita walipata mafunzo ya mfumo mpya wa ununuzi wa umma kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzo wa Umma (PPRA) yaliyofanyika mjini Dodoma,ambayo yalishirikisha wataalam 180 kutoka Sekretarieti za mikoa yote 26 ya Tanzania Bara.
Akizungumza wakati anafungua mafunzo hayo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Jumanne Mwankhoo amesma PPRA imeunda mfumo mpya wa ununuzi wa umma unaoitwa National eprocurement Sytem of Tanzania (NeST) ambao umeanza kutumika Julai Mosi mwaka huu ambapo serikali imeridhia kuanza kutumika mfumo mpya wa ununuzi kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu.
Amesema serikali imepitisha sheria ya kuanza kutumika mfumo mpya wa ununuzi wa umma NeST baada ya kubaini changamoto za kiufundi zilizojitokeza kwenye mfumo wa ununuzi wa awali (TANePS) na lengo la serikali ni kuhakikisha,Halmashauri,Mikoa na Taasisi zote zinaanza kutumia mfumo wa NeST.
“Ninyi wataalam sita kutoka kila Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma mtakwenda kuwa walimu wa mfumo mpya wa ununuzi NeST wa wataalam wengine waliopo kwenye Halmashauri zenu ili kila mtaalam aweze kuufahamu vizuri na kuanza kuutumia mfumo huu’’,alisistiza.
Kwa upande wake Msimamizi wa mafunzo hayo Piniel Mbura akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo amesema,utafiti umebaini kuwa mfumo mpya wa ununuzi wa umma NeST una faida nyingi zikiwemo kuongeza wigo wa ushiriki kwenye ununuzi, uwajibikaji,kupunguza muda wa mchakato,upatikanaji wa taarifa na kupunguza mianya ya rushwa.
Faida nyingine amezitaja kuwa ni uandaaji wa zabuni zote na uombaji wa zabuni utafanyika ndani ya mfumo,wazabuni ndani ya mfumo watajisajiri na kupandisha nyaraka zao zote kwa mara moja na nyaraka zote zitasainiwa ndani ya mfumo.
Sekta ya ununuzi wa umma inachukua takriban asilimia 70 ya Bajeti ya Serikali hivyo ununuzi wa umma ni eneo nyeti kwa sababu serikali inatenga fedha nyingi ili kufanikisha malengo na matarajia ya nchi kwenye ununuzi.]
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.