• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MFUMO wa stakabadhi ghalani ulivyoimarisha ushirika na kuinua wakulima mkoani Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: August 9th, 2020


Wakulima  mkoani Ruvuma wamenufaika na bei kwa utaratibu  wa mfumo wa stakabadhi ghalani  hali iliyowezesha kuuza mazao kwa bei nzuri na kupata faida.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema  kabla ya mfumo huo bei ya Ufuta ilikua shilingi 1,500, Soya Tshs.500 kwa kilo na Mbaazi ilikuwa shilingi kati ya shilingi 100 na 200 kwa kilo moja.

Amesema  baada ya kuanza kuuza mazao hayo kwa mfumo wa stakabadhi ghalani Ufuta umepanda bei toka shilingi 1500 hadi 4,110 kwa kilo na kwamba Mauzo hayo yaliwawezesha wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kupata kiasi cha shilingi bilioni 24 kutokana na mauzo ya zao la ufuta pekee.Amesema wakulima kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani katika zao la soya walifanikiwa kuuza kilo moja toka shilingi500 hadi hadi kufikia shilingi 850 kwa kilo moja  na mbaazi toka shilingi 150  kwa kilo hadi  shilingi 850.

“Mfumo huu wa stakabadhi za ghalani umeleta tija kwa wananchi na hivyo kuongeza uzalishaji kutoka tani 8,000 hadi 10,000 za zao la ufuta na Kufufuliwa kwa vyama vya Ushirika vya kilimo na Masoko kwani kabla ya kuanza mfumo  huu vyama vilivyokuwa vinafanya kazi ni 67  na baada ya mfumo huu kuanzishwa vyama vinavyofanya kazi ni 204 ‘’,alisema Mndeme.

Hata hivyo Mndeme amesema Halmashauri mkoani Ruvuma zimepata na zinaendelea kupata ushuru na kukuza mapato ya ndani ambapo takwimu za uzalishaji na mapato ya wakulima kwa sasa ni rahisi kupatikana na kuwa wazi tofauti na kabla ya utekelezaji wa mfumo wa stakabadhi ghalani.

 Amesema mfumo wa Stakabadhi ya mazao ghalani unatekelezwa katika mazao sita ambayo ni korosho, Kahawa, Tumbaku, ufuta, mbaazi na Soya na kwamba umeweza kuingiza fedha kiasi cha shilingi  634,797,630,064 kutokana na mauzo hayo.

Uzalishaji wa mazao yanayouzwa kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo zao la korosho mwaka 2015 uzalishaji ulikuwa tani 11,329,800 zenye thamani ya shilingi 13,594,800,000 ukilinganisha na mwaka 2020 uzalishaji umeongezeka hadi kufikia tani 24,625,824 zenye thamani ya shilingi  65,376,990,905.

“Zao la Kahawa mwaka 2015 uzalishaji ulikuwa tani 17,518,500 zenye thamani ya shilingi 66,570,300,000 na kwa mwaka 2019/2020 uzalishaji ni Tani 15,675,100 zenye thamani ya shilingi 64,048,458.600.

Amesema zao la tumbaku kwa mwaka 2016/2017 uzalishaji ulikuwa tani 160,855 zenye thamani ya shilingi 542,323,900 na kwa mwaka 2018/2019 uzalishaji wa tumbaku ulikuwa ni tani 1,247,814.75 zenye thamani ya shilingi 4,101,640,347.

Mndeme amelitaja zao la Ufuta uzalishaji mwaka 2018//2019 ulikuwa tani 8,428,268 zenye thamani ya shilingi 24,882,415,441 na kwa mwaka 2019/2020 uzalishaji ulikuwa ni tani 10,909,667 zenye thamani ya shilingi 23,687,790,987 na kwamba Ununuzi wa zao hili bado unaendelea.

Akizungumzia uendelezaji wa Miradi ya Kiuchumi ya vyama vya Ushirika,Mkuu wa Mkoa amesema,Serikali kupita vyama vya Ushirika imetekeleza na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi ambapo jumla ya fedha kiasi cha Tsh 1,128,141,200 zinatekeleza miradi mbalimbali.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni Ujenzi wa kiwanda cha vifungashio cha chama kikuu SONAMCU Ltd wilayani Namtumbo,ukarabati wa ghala la chama kikuu cha TAMCU Ltd  wilayani Tunduru na ukarabati wa maghala matano  kati ya saba ya chama kikuu cha MBIFACU Ltd wilayani Mbinga  na Ukarabati wa  hoteli ya MBICU mjini Mbinga.

 Ameitaja miradi mingine kuwa ni ununuzi wa magari  matatu ya mizigo kwa ajili ya usafirishaji wa mazao ya kilimo ya wakulima kwa vyama vya Msingi Mruji, Mtiti na Sama vilivyopo Wilaya ya Tunduru na usimamizi wa uendelezaji wa Mradi wa kiuchumi wa shamba la kahawa la chama kikuu cha MBIFACU Ltd , Ujenzi wa Mradi wa shule ya Sekondari ya Mahenge AMCOS Ltd wilayani Mbinga na  Ujenzi wa ghala la kuhifadhia mazao ya wakulima la chama cha Msingi Kimuli (AMCOS).

Amesema Mkoa Ruvuma una jumla ya vyama vya Ushirika 296, kati ya hivyo AMCOS 201, vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) 92 na vyama vikuu (union) 3 ambavyo ni TAMCU Ltd, SONAMCU Ltd, NA MBIFACU LtD) na kwamba Mkoa ulikuwa na AMCOS 237 mwaka 2015 ikilinganishwa na AMCOS 296 mwaka 2020.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Agosti 9,2020

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.