Wakulima wa soya chama cha Msingi cha ushirika cha Lina Amcos katika kijiji cha ndogosi wilaya Songea, mkoani Ruvuma.
Wameeleza namna mfumo huo unavyo wapa faida kwenye kilimo cha soya, wamekiri kuuza mazao kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kumewaletea faida kubwa ikiwemo kuuza kwa bei nzuri.
Akizungumza kwaniaba ya wanakikundi, katibu wa kikundi hicho Basilius komba, ameeleza kuwa mfumo huo ulivyo wasaidia kuwakwepa makanjanja na sasa moja kwa moja wanaleta ushirika kwaajili ya kuuza.
“Lakini kwasasa naona tunafaidika kwasababu stakabadhi ghalani umetunufaisha hata bei zimekuwa rafiki haituumizi sana, sababu tunatoa mazao shambani nakuleta ushirika kwahiyo wao ndio shugulikia kuuza na kingine tunapa fedha zetu kwa wakati” alisema Komba.
Hata hivyo ameiomba serikali kuboresha kwenye upangaji bei ili kuwasaidia wao wakulima wafahamu mapema , pia amewashauri wakulima ambao awatumii mfumo hou wabadilike kwani unamanufaa sana kwa wakulima
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.