Wakulima wa Mbaazi wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wameingiza zaidi ya bilioni 10 katika mauzo ya zao la Mbaazi kwa njia ya mfumo Stakabadhi ghalani, baada ya kufanyika kwa minada mitano ya zao hilo kwa msimu wa 2023/2024.
Meneja mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru Ndg .Imani Kalembo, amesema kwa msimu huu wa mauzo ya zao la Mbaazi Chama Kikuu kimefanya minada mitano, ambapo tani zisizopungua 5,000 zimeuzwa na kuingiza zaidi ya shilingi bilioni 10 .
Meneja Kalembo amesema matarajio ya Chama Kikuu cha Ushirika Tunduru ni kukusanya zaidi ya tani 8,000 kwa msimu ujao wa zao la mbaazi, kutokana na mikakati iliyowekwa na kuahidi kuzalisha mazao yaliyo bora ya Stakabadhi ghalani ikiwemo Ufuta, Mbaazi na Korosho
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.