Mkoa wa Ruvuma umeendelea kuwa na usalama wa chakula kwa zaidi ya miaka kumi na mbili mfululizo, ukiwa na ziada ya tani 1,485,763.76 za chakula.
Afisa Kilimo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Onesmo Ngao anasema Katika msimu wa 2023/2024. Mkoa ulizalisha tani 1,955,763.76 za mazao ya chakula dhidi ya mahitaji ya tani 470,000, hivyo kuzidi mahitaji kwa kiwango kikubwa.
Hali hii imeufanya Mkoa wa Ruvuma kuendelea kuongoza kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya chakula, hususan zao la mahindi.
Ngao anasema Kwa msimu wa kilimo wa 2024/2025, mkoa umepanga kulima hekta 1,379,036 za mazao ya chakula, biashara na bustani, ukitarajia mavuno ya tani 2,158,704. Kati ya hizo, hekta 998,745 ni za mazao ya chakula yatakayotoa tani 1,842,503, huku hekta 363,055 zikihusisha mazao ya biashara yenye matarajio ya tani 101,252.
Katika msimu wa kilimo wa 2023/2024, mkoa ulizalisha jumla ya tani 2,052,449.09 za mazao, ambapo tani 1,955,763.76 zilikuwa za mazao ya chakula na tani 96,685.33 za mazao ya biashara.
Katika msimu huo,Mkoa ulilenga kulima hekta 1,006,325, huku matarajio yakiwa mavuno ya tani 2,168,041. Hekta 642,906 zilitengwa kwa kilimo cha mazao ya chakula, zikitarajiwa kuzalisha tani 1,882,473, huku hekta 348,441 zikihusisha mazao ya biashara yenye matarajio ya tani 100,557. Mazao ya bustani yalihusisha hekta 14,978, yakitarajiwa kutoa tani 185,012.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwezesha upatikanaji wa pembejeo, ambapo hadi tarehe 31 Desemba 2024, jumla ya tani 82,120 za mbolea ziliingizwa katika mkoa wa Ruvuma. Kati ya hizo, tani Zaidi ya 55,488.886 tayari zimesambazwa kwa wakulima, huku mahitaji yakiwa tani 113,000.
Mkoa unaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati ili kuongeza uzalishaji wa mazao msimu ujao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.