MIKATABA ya utoaji huduma jumuishi za UKIMWI na kifua kikuu kupitia mradi wa USAID Afya yangu Kanda ya Kusini katika kipindi cha mwaka 2024/2025 imesainiwa mkoani Ruvuma.
Hafla ya kusaini mikataba hiyo imeshirikisha wakurugenzi wa Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma na kufanyika kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea ambapo mgeni rasmi aliikuwa ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Joel Mbewa.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mbewa amesema Utekelezaji Wa Bajeti ya mwaka 2024/2025 kupitia Mradi wa USAID AFYA YANGU Kanda ya kusini kwa ngazi ya Mkoa, Halmashauri na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, wanatekeleza afua za UKIMWI,Kifua Kikuu na huduma jumuishi za uzazi wa Mpango na Jinsia.
“Katika kipindi cha mwaka 2024/2025 Serikali ya Marekani imetenga jumla ya fedha kiasi cha TZS.4,14,873,990.55 kwa ajili ya kusaidia shughuli za utoaji wa huduma za UKIMWI na Kifua Kikuu kupitia Mamlaka ya Mkoa, Halmashauri zote Vituo vya Mashirika ya Dini na Asasi ya kiraia ya ROA’’,alisema
Amesema Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) na Shirika na Maendeleo la Marekani (USAID) kupitia Mradi wa USAID Afya Yangu Kanda ya Kusini, inasaidia Vituo 135 Sawa na asilimia 89.4 kati ya 151 vinavyotoa Huduma za Kliniki ya Tiba na Matunzo (CTC) Katika Mkoa.
Amebainisha kuwa kati ya fedha zitakazotolewa kiasi cha TZS.3,072,313,570.85 Sawa na asilimia 74.2 zitatolewa kwa Taasisi za Serikali ukiwemo Mkoa na Halmashauri zake zote.
Hata hivyo amesema kiasi cha shilingi 259,915.70 sawa na asilimia 6.2 zitatolewa kwa vituo viwili vya Mashirika ya Dini (FBO), na shilingi 810,311,504.00 sawa na asilimia 19.6 zitatolewa kwa Asasi ya Kiraia ya ROA inayofanya kazi Katika Halmashauri zote.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Hilda Ndambalilo, amesema Mradi wa USID Afya Yangu Kanda ya Kusini unalenga kusaidia na Serikali ya Tanzania Kutoa Huduma bora jumuishi za matunzo , matibabu, na kuzuia maambukizi ya VVU na Kifua Kikuu ambazo zitaboresha matokeo chanya ya afya, hasa kwa vijana na watoto
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.