SERIKALI imeleta fedha kiasi cha shilingi Milioni 141 kwaajili ya ujenzi wa Bweni katika Shule ya Sekondari Ifinga.iliyopo Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma
Hayo amesema Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata yaLituta na Mahanje wakati wa uzinduzi wa Soko la Kisasa linalojengwa kupitia mradi wa TASAF.
“ Serikali inafikilia kujenga miundo mbinu Mbunge wenu amepambana ndiomana miundombinu inaboreshwa,na tumeletewa fedha Milioni 141 kwaajili ya ujezi wa Bweni Ifinga”.
Ndile amesema ujenzi wa Bweni katika Shule ya Sekondari Ifinga litasaidia wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Halmashauri hiyo kwenda kusoma Ifinga na wanafunzi wa Ifinga kubadilisha mazingira kusoma maeneo mengine.
“Shule ya Sekondari Ifinga inajumla ya wanafunzi 73 ikiwa wanafunzi hao wanamaliza shule ya Msingi na kujiunga na Shule ya Sekondari katika kijiji hicho”.
Hata hivyo kwa upande wake Afisa Elimu Maalumu Tedy Sanga amesema Serikali imeleta fedha kiasi cha shilingi Milioni 128 kwa ajili ya ujenzi wa Bweni katika Shule ya Msingi Madaba kwa ajili ya wanafunzi maalumu. na kwamba bweni hilo litasaidia wanafunzi maalumu kutoka maeneo mbalimbali ya Halmashauri kuishi na kusoma katika mazingira raf
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.