Mkuu wa wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa, Wakili Julius S. Mtatiro amekagua maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa kituo cha Afya Juma Homera, kilichopo kata ya Nakayaya wilayani humo.
Kituo hicho cha afya kilianza kujengwa chini ya usimamizi wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Juma Homera, ambaye kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Mbeya. Mh. Homera alikutana na wadau mbalimbali ambao walichangia na kuunda kamati za usimamizi ili kuanzisha ujenzi wa kituo hicho.
Ujenzi na ukarabati wa mradi huo unagharimu zaidi ya shilingi milioni 200, fedha ambazo zimetokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, ambao unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Januari mwaka 2024.
Mh. Wakili Mtatiro aagiza kampuni ya usambazaji wa umeme (TANESCO) kuhakikisha wanarejesha Transfoma waliyoiondoa maeneo ambayo mradi huo wa ujenzi na ukarabati unaendelea.
“Ninafahamu kwamba TANESCO Tunduru walikumbana na changamoto mbalimbali ndio maana wakaondoa Transfoma iliyokuwa maeneo haya ambayo Mradi wa kituo chetu cha afya unaendelea” Alisema Mh. Mtatiro, “Namwagiza Meneja wa TANESCO Tunduru atafute mbadala wa Transfoma hiyo ili kusaidia mradi huu kukamilika kwa muda uliopangwa”
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Daktari Renatus Mathias, ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuiwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, vilevile amemshukuru Mbunge wa Tunduru Kaskazini Mh. Hassan Zidadu Kungu pamoja na waheshimiwa madiwani wote.
Ujenzi na ukarabati wa kituo cha afya Juma Homera upo katika hatua ya umaliziaji, ujenzi wa kituo hicho ni moja kati ya mikakati ya serikali ya awamu ya sita chini ya Raisi wake Mheshimiwa, Daktari, Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za afya zilizo bora.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.