WANANCHI wa kijiji cha Lyangweni kata ya Litapaswi Halmashauri ya wilaya Songea mkoani Ruvuma,wameanza kupata huduma ya maji ya bomba kwa mara ya kwanza tangu nchi ipate Uhuru.
Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Songea, kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji ya bomba uliogharimu Sh.milioni 618.
Kukamilika kwa mradi huo,ulianza kutoa huduma ya maji kwa wananchi 2,159 wa kijiji hicho kumeleta nafuu kubwa kwa wananchi ambao kwa muda mrefu walitembea zaidi ya kilomita 3 kila siku kwenda kuchota maji kwenye mito na vyanzo vingine vya asili.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lyangweni Menrald Komba amesema ,kukamilika kwa mradi huo kumewaondolea mateso makubwa wananchi kwa kutembea umbali mrefu kila siku kwenda kutafuta maji.
Mwalimu MKuu wa shule ya Msingi Kilawalawi Herman Komba ameishukuru serikali kupitia RUWASA kwa kuwatua ndoo kichwani wakiwemo wanafunzi ambao walisafiri umbali mrefu kusaka maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.