Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mheshimiwa Siomn Chacha amefungua rasmi msimu wa Ukusanyaji wa Ufuta kwa ajili ya mauzo ya zao la ufuta.
Hayo yamesemwa wakati wa Mkutano wa wadau wa zao la ufuta uliofanyika wilayani humo ambao ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani, viongozi wa Vyama vya Msingi, mameneja na makarani wapimaji.
Chacha amesisitiza viongozi wa AMCOS na makarani kusimamia ukusanyaji wa ufuta kwa uadilifu ili kuleta tija kwa wakulima wa zao hilo.
“tunapokwenda kusimamia Ukusanyaji wa zao hili , tunatakiwa kuwa na vitu vitatu, ambavyo ni uadilifu, uaminifu na ushirikiano baina yetu”,alisema DC Chacha.
Ameongeza kuwa minada ya ufuta wilayani Tunduru itafanyika kidijitali kupitia mfumo wa Soko la Bidhaa (TMX) kwa kushirikiana na Chama Kikuu cha Ushirika wa Masoko ya Mazao Tunduru (TAMCU LTD).
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.