Miti adimu duniani ambayo inapatikana wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ni miti mawe ambayo ni jamii ya miti ya mitetereka ambayo katika dunia nzima inapatikana katika nchi mbili za Tanzania wilaya za Tunduru na Namtumbo mkoani Ruvuma na nchini Marekani.
Miti hii inapatikana katika kijiji cha Mbati wilayani Tunduru na kijiji cha Likuyu wilayani Namtumbo.
Miti hii ni jamii ya miti ya mitetereka. Mti mawe unaweza kuishi kwa zaidi ya miaka 120 changamoto kubwa inayoikabili miti hiyo ni kushambuliwa na watu wengi hivyo ipo katika hatari ya kutoweka.
Kuwepo kwa kivutio cha miti mawe kunaonesha kuwa ukanda wa kusini mwa Tanzania kuna utajiri wa vivutio vya utalii ambavyo havipatikani sehemu nyingine yeyote nchini hivyo vivutio hivyo vikiibuliwa na kutangazwa vinaweza kufungua fursa za utalii kusini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.