• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MJI wa Peramiho unavyoutangaza Mkoa wa Ruvuma kimataifa

Imewekwa kuanzia tarehe: August 15th, 2024

Mji wa Peramiho uliopo Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa miji ya zamani yenye historia ya kipekee katika ukanda ya kusini.

Mji wa huo unafahamika zaidi nje ya nchi pengine kuliko miji mingine iliyopo kusini mwa Tanzania kutokana na mji huo kuwa na historia ya namna yake kipekee ikiunganisha Tanzania na mataifa ya Ulaya.

Historia ya mji wa Peramiho uliopo kilometa 24 tu kutoka makao makuu ya mkoa wa Ruvuma Songea inaunganishwa na wabenediktini wa kanisa katoliki kutoka St.Otilia nchini Ujerumani, ambao waliamua kuweka makao makuu yao katika Abasia ya Peramiho.

Wabeneditine hao waliingia kwa mara ya kwanza katika mji huo mkongwe mwaka 1898 wakiongozwa na Kasian Spiss. Tangu wakati huo wabenediktine hao wamekuwa wakifanya mambo yanayoutangaza mji huo hali iliyosababisha kuutambua mji wa Peramiho kuwa ni mji unaokidhi vigezo kuwa mji wenye utalii wa kiutamaduni.

Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho ya Taifa Philipo Maligisu anasema  wabenediktine wa Abasia ya Peramiho wametengeneza historia ya kipekee na kuvutia katika nchi ya Tanzania ambao wameacha historia katika mji wa Peramiho na taifa kwa ujumla hasa walipojikita katika suala zima la elimu na kuamua kuwekeza katika elimu  kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Historia inaonesha kuwa walipoingia kwa mara ya kwanza wabenediktine hao kwa kutambua umuhimu wa elimu waliamua kuanzisha madarasa kwa kufundisha walimu na kufundisha wanafunzi hivyo kufundisha elimu zote mbili yaani elimu ya kiroho na elimu dunia

Kwa msingi huo eneo la Peramiho katika historia ya Tanzania ina historia ya kipekee kwa zaidi ya miaka 100 hivyo kuna ushahidi ambao unaonesha wabenediktine walidhamiria kufanya mambo ya msingi katika mji wa Peramiho na taifa kwa ujumla.

Utafiti uliofanywa katika mji wa Peramiho unaonesha kuwa wabenediktine hao walizindua rasmi mji huo Julai 31,1898 na tangu hapo waliendelea na shughuli zao wakiwa na mahusiano mazuri wakati huo na utawala wa machifu katika eneo hilo.

Hata hivyo mahusiano hayo mazuri baina ya wabenedikitine hao kutoka nchini Ujerumani na machifu ulikuja kuharibika wakati wa vita ya Majimaji ambayo vilianza mwaka 1905 na kumalizika mwaka 1907 na kusababisha padre Fransis Scuss wa Abasia hiyo kuuawa Septemba 9 1905.

Baada ya kumalizika vita hiyo, ilijitengeneza tena historia mpya ya kanisa la Abasia ya Peramiho hivyo kulichukulia eneo hilo kama eneo la kipekee kwa kuzingatia misingi ya sheria ya Tanzania namba 10 ya mwaka 1964 na maboresho yake namba 22 ya mwaka 1979 ambayo inayatambua maeneo yote ya kihistoria kulingana na umuhimu wake katika jamii.

Wananchi wa Ujerumani  wanaijua Peramiho pengine kuliko hata sisi watanzania,ndiyo maana  kizazi na kizazi wanasafiri kwa gharama kubwa hadi katika mji huo ili kufanya utalii wa kiutamaduni kwa kutembelea katika maeneo mbalimbali ya kihistoria ili kujifunza mambo mbalimbali.

Sera ya Taifa ya utamaduni ya mwaka 1997  ina tamka bayana kuwa  eneo lolote la kihistoria linapokuwa limetimiza miaka 100 tayari moja kwa moja linaingia katika urithi wa utamaduni wa  taifa.

Kutokana na hali hiyo ukiangalia mji huo wa Peramiho tayari umekidhi vigezo na maeneo yake yote ya kihistoria kuingia katika urithi wa utamaduni wa taifa kwa ajili ya kujifunza elimu na utalii

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.