Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamemuonesha eneo la Ujenzi wa Bandari ya Mbamba bay inayogharimu shilingi bilioni 80,Mkandarasi wa Kampuni Xiamen Ongoing Construction Group Ltd na kumtaka aanze kazi ya Ujenzi.
Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Manga Gassaya amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anakamilisha kazi baada ya miezi 24.
Amemtaka Mkandarasi huyo kuwatumia wananchi wa Nyasa Kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kutoa fedha ya UJENZI wa bandari ya Mbamba bay itakayokuwa makao makuu ya Bandari zote za ziwa Nyasa na kuunganisha Nchi za Malawi na Msumbiji.
Mkandarasi ameahidi kutekeleza mradi huo kulingana na mkataba ili wananchi waweze kunufaika na bandari hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.