Mkoa wa Ruvuma umefikia asilimia 82 ya lengo la kuhesabu kaya 450,000.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakati anakagua mwenendo wa sensa katika vijiji vya Kitanda Wilaya ya Mbinga na kijiji cha Linda Wilaya ya Nyasa
Amelitaja lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anahesabiwa .
”Kwa taarifa za kitaifa za asubuhi ya Agosti 27 Mkoa wa Ruvuma tumeshahesabu kaya kwa zaidi ya asilimia 82”,alisema Kanali Laban.
Hata hivyo amesema kwa muda uliobaki Mkoa unaweza kufikia lengo la kuhesabu kaya zaidi ya 450,000.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangasongo alisema Halmashauri ya Mji Mbinga ilitarajia kuhesabu kaya zaidi ya 33,000 ambapo hadi sasa kaya zaidi ya 27,000 zimehesabiwa
Mheshimiwa Mangasongo amesema Katika Wilaya ya Nyasa yenye kata 18 hadi kufikia Agosti 27,kata 16 zimehesabiwa na makarani wanakamilisha kazi ya kuhesabu kata mbili zilizobakia.
Sensa ya watu ilianza nchini kote Agosti 23 na inatarajia kukamilika Agosti 29.
Imeandikwa na Albano Midelo,Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.