• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma kukusanya chupa za damu 14,789

Imewekwa kuanzia tarehe: June 4th, 2025

Mkoa wa Ruvuma unashiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Wiki ya Uchangiaji wa Hiari wa Damu Salama, ambayo yameanza tarehe 1 Juni na yatakayofikia kilele chake tarehe 14 Juni 2025.

Maadhimisho haya ni sehemu ya kampeni ya kimataifa inayolenga kuhakikisha upatikanaji wa damu salama kwa watu wote wanaohitaji huduma hiyo muhimu ya kiafya.

Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea, Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amesema Serikali kupitia mkoa huo imejipanga kuimarisha huduma za afya kwa hatua mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya, ununuzi wa dawa, vifaa vya uchunguzi, pamoja na majokofu ya kuhifadhia na kusafirisha damu.

Kaulimbiu ya mwaka huu ya maadhimisho haya ni “Changia Damu, Leta Matumaini, Pamoja Tunaokoa Maisha”, ambayo inasisitiza umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari kama njia ya kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.

Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa kutoka Januari hadi Mei 2025, Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kukusanya jumla ya chupa 2,952 za damu, ambayo ni sawa na asilimia 20 ya lengo la chupa 14,789 kwa mwaka huu.

Hata hivyo hali hiyo inaonesha bado kuna upungufu mkubwa wa damu na hivyo kuhitajika juhudi za pamoja katika uhamasishaji na uchangiaji wa damu.

Bi. Makondo ametoa wito kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma kuhakikisha kuwa Kamati za Damu Salama zinatengewa bajeti ya kutosha kwa ajili ya shughuli za uhamasishaji, hasa katika shule, vyuo, taasisi na mashirika mbalimbali.

Amelitaja lengo kuu ni kuongeza uelewa na kuimarisha utamaduni wa kuchangia damu ili kila halmashauri iweze kufikia lengo la ukusanyaji damu salama kwa asilimia 100 kama ilivyopendekezwa na Wizara ya Afya.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dr. Louis Chomboko, ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia damu katika maeneo yote yatakayopangwa kutoa huduma hiyo ndani ya kipindi cha wiki hii ya maadhimisho.

“Kuchangia damu ni tendo la huruma, uzalendo na upendo kwa maisha ya wengine. Tunapotoa damu, tunaleta matumaini mapya kwa wagonjwa waliolazwa na wanaohitaji upasuaji, wajawazito, watoto na waathirika wa ajali,” amesema Dr. Chomboko.

Maadhimisho haya yanatarajiwa kuchochea mwitikio chanya wa wananchi na taasisi mbalimbali katika kujenga jamii inayothamini umuhimu wa damu salama kwa ustawi wa afya ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • NMB yatoa madawati 150 ya milioni 16 Songea

    June 05, 2025
  • UCHANGIAJI damu wazidi kuimarika Ruvuma

    June 04, 2025
  • TRILIONI 1.18 za Rais Samia zavunja ukame wa maendeleo Ruvuma,ndani ya miaka minne Ruvuma yachanua

    June 04, 2025
  • RAS RUVUMA alivyowaongoza wananchi kuchangia damu

    June 04, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.