• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma kulima zaidi ya hekta 900 za mazao mbalimbali

Imewekwa kuanzia tarehe: January 26th, 2023

 

MKOA wa Ruvuma umelenga kulima jumla ya hekta 930,082 za mazao ya chakula,biashara na mazao ya bustani katika msimu wa kilimo wa mwaka 2022/2023.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema hekta hizo zinatarajia kutoa mavuno ya tani 1,965,072 na kwamba kati ya hekta hizo,kilimo cha mazao ya chakula ni hekta 569,070 zinazotarajia kutoa mavuno ya tani 1,638,808.

Amesema katika mazao ya biashara zinatarajiwa kulimwa hekta 337,572 ambazo zinazotarajiwa kutoa mavuno tani 102,379  na kwa mazao ya bustani zinatarajiwa kulimwa hekta 23,399 zinazotarajiwa kutoa mavuno tani 223,886.

Hata hivyo amesema hali ya upatikanaji wa chakula mkoani Ruvuma ni nzuri kwa kuwa ipo katika kiwango cha utoshelevu na ziada kwa miaka 12 mfululizo.

“Chakula kilichozalishwa katika msimu wa 2021/2022 kinatumika kwa msimu huu wa  2022/2023 ambapo mazao ya chakula yalizalishwa tani 1,256,362 na mahitaji ya chakula ndani ya Mkoa kwa msimu wa 2022/2023 ni tani 469,172 na kuufanya Mkoa kuwa na ziada ya chakula tani 787,190’’,alisema Kanali  Thomas.

Akizungumzia upatikanaji wa mbolea ya ruzuku mkoani Ruvuma,Kanali Thomas amesema katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA) unatekeleza mpango wa utoaji  mbolea ya ruzuku.

Amesema hadi kufikia Januari 13,2023,Mkoa wa Ruvuma kupitia vitabu umesajili jumla ya wakulima 278,010 kati ya lengo la kusajili wakulima 428,288 na kwamba jumla ya wakulima 272,624 wameshaingizwa kwenye mfumo sawa na asilimia 98 na walianza kupata mbolea tangu Agosti 2022 zoezi la usajili lilipoanza.

Hata hivyo amesema katika msimu wa mwaka 2022/2023 Mkoa wa Ruvuma umelenga kusambaza mbolea ya ruzuku zaidi ya tani 50,000 ambapo hadi sasa Mkoa umesambaza zaidi ya tani 42,000 kupitia Kampuni  na mawakala wa mbolea.

Mkoa wa Ruvuma kwa miaka minne mfululizo umeendelea kuwa kapu la chakula la Taifa baada ya kuongoza kitaifa katika uzalishaji wa chakula nchini.

Imeandikwa na Albano Midelo wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma

Januari 26,2023

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.