• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma ulivyoimarisha huduma za afya katika ngazi zote

Imewekwa kuanzia tarehe: March 30th, 2025

Mkoa wa Ruvuma unazidi kupiga hatua katika kuboresha sekta ya afya, ambapo Kwa jumla, mkoa  una vituo 473 vya kutoa huduma za afya, vinavyojumuisha hospitali, vituo vya afya, na zahanati zinazosimamiwa na Serikali, Mashirika ya Dini, na sekta binafsi.

Muundo wa Vituo vya Afya

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Louis Chomboko anasema  Ruvuma una hospitali 18, ambapo hospitali tisa zinamilikiwa na Serikali, saba ni za Mashirika ya Dini, huku hospitali mbili  zikimilikiwa na watu binafsi.

Mkoa una vituo vya afya 50, ambapo asilimia kubwa ikiwa ni vituo vya afya 39 vinamilikiwa na Serikali, huku 11 vikiwa chini ya Mashirika ya Dini na sekta binafsi.

Kwa upande wa zahanati, mkoa una jumla ya 341, kati ya hizo 277 zinamilikiwa na Serikali na 64 zinamilikiwa na sekta binafsi pamoja na Mashirika ya Dini. Muundo huu wa vituo vya afya unalenga kuhakikisha huduma zinapatikana kwa wananchi wa maeneo yote ya mkoa.

Changamoto ya Upatikanaji wa Rasilimali Watu

Pamoja na uwepo wa vituo vingi vya afya, upungufu wa watumishi wa afya ni moja ya changamoto kubwa inayoukabili mkoa. Kwa sasa, kuna watumishi wa afya 3,323, sawa na asilimia 47.2 ya mahitaji halisi ya watumishi 7,043.

 Ongezeko la vituo vipya vya huduma limechangia kupungua kwa uwiano wa watumishi waliopo katika ngazi mbalimbali za utoaji huduma. Hali hii inasababisha msongamano kwa watumishi waliopo na kupunguza ufanisi wa utoaji huduma za afya kwa wananchi.

Matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki wa Serikali (GoTHOMIS)

Katika jitihada za kuimarisha utoaji wa huduma za afya, Serikali imeanzisha matumizi ya Mfumo wa Kielektroniki wa GoTHOMIS kwa lengo la kuboresha utunzaji wa kumbukumbu za wagonjwa na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Hadi kufikia Desemba 2024, jumla ya vituo 307 kati ya 325 vya serikali vilikuwa vimesimikwa mfumo huu, ikiwa ni asilimia 94.5.

Mkoa wa Ruvuma umeonesha dhamira ya dhati ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake. Uwepo wa vituo vingi vya afya, pamoja na jitihada za kuboresha mifumo ya kielektroniki, ni hatua muhimu katika safari ya kuimarisha sekta ya afya mkoani hapa.

 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • BODI ya kwanza ya maji yazinduliwa Tunduru

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.