Mkoa wa Ruvuma unaendelea kuchukua hatua madhubuti za kupambana na ugonjwa wa homa ya nyani (Mpox).
Hayo yameelezwa na Mratibu wa Huduma za Chanjo Mkoa wa Ruvuma Winbroad Mvile kwenye kikao cha tathmini ya lishe, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Mvile ameutaja ugonjwa wa Mpox kuwa unasababishwa na virusi ambavyo kwa sasa havina tiba, na njia pekee ya kupambana nao ni kuchukua tahadhari za kujikinga, ikiwemo kuepuka kugusana na wanyama au watu waliopata maambukizi.
"Mkoa wa Ruvuma umechukua hatua kadhaa kupambana na kuzuia Ugonjwa wa Mpox halmashauri zote za Mkoa zimeagizwa kujiandaa dhidi ya ugonjwa wa Mpox’’, alisema.
Hata hivyo amesema timu za ufuatiliaji wa Mpox zinafanya ufuatiliaji ili kufahamu kama Kuna dalili za uwepo wa ugonjwa huu katika mkoa wa Ruvuma.
Amebainisha kuwa hadi sasa, hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitishwa kuwa na maambukizi ya Mpox nchini ingawa nchi jirani kama Congo na Uganda tayari zimekuwa na visa vya ugonjwa huu
Amesema elimu juu ya ugonjwa wa Mpox na namna ya kujikinga nayo imeshatolewa katika taasisi za serikali na mikusanyiko mbalimbali, ili kuhakikisha jamii inatambua athari zake na namna ya kujikinga
Amebainisha kuwa halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma zimetenga wodi maalum kwa ajili ya kuwahudumia waathirika wa Mpox, endapo watabainika.
Mpox ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Mpox ambapo awali ugonjwa huo ulijulikana kama ugonjwa wa monkey pox (ugonjwa wa nyani) na virusi hivi kwa kawaida ushambulia wanyama hususani nyani na panya.
Mratibu wa Huduma za Chanjo Mkoa wa Ruvuma Winbroad Mvile
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.