MKOA wa Ruvuma, kupitia ofisi ya maendeleo ya michezo, utamaduni na vijana, imepanga mikakati ya kuibua vipaji mashuleni mkoani umo.
Hayo yameelezwa na afisa maendeleo ya michezo, utamaduni na vijana, wa Mkoa wa Ruvuma, Antony Luoga, ameeleza namna mkoa ulivyo amua kutilia mkazo kwenye kuibua vipaji mashuleni
Alisema mkoa umepanga kusisitiza somo la elimu ya michezo kufundishwa kila shule, pia kusisitiza michezo ifanyike mara kwa mara na kwakufanya hivyo tutaweza kuhibua vipaji vingi na kama serikali tunaweza kuviendeleza.
“Na hiyo itasaidia kutoa fursa kwa wanafunzi mara kwa mara kujifunza sheria za mchezo husika, lakini pia kupata ujuzi ambao utasaidia uendelezaji wa vipaji vya hawa watoto, lakini kuusaidia mkoa kufanya vizuri katika mashindano yake mbalimbali”alisema Luoga.
Luoga amewaomba wadau mbalimbali ambao wanao uwezo wa kuibua vipaji na kuviendeleza vili vile kuunga mkono serikali, pamoja kwamba michezo ujenga afya lakini kwa kiasi kikubwa sasa ni ajira hivyo wito wa serikali tunaomba wadau kuweza kujitokeza kushirikiana na serikali katika kuendeleza vipaji
Alisema serikali inatambua changaomoto za miundo mbinu kwa michezo mbalimbali, kama mkoa tumeanza kisisitiza kila halmashauri, waweze kuboresha miundo mbinu, lakini kama mkoa tumetapa shule tatu ili kuendeleza vipaji vya wanafunzi
Hata hivyo aliongeza kusema kama mkoa wameitenga shule maalumu ya maanje sekondari, kuwa ni shule ya michezo ambapo wanafunzi wote waliofikia levo ya kitaifa katika mashindano watachukuliwa na kupelekwa uko asa wanao faulu shule za msingi wapelekwe kuendeleza vipaji vyao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.