Mkoawa Ruvuma umeendelea kuwa mzalishaji mkubwa wa mazao ya nafaka nchini,ukizalisha jumla ya tani 2,052,449.09 za mazao katika msimu wa 2023/2024.
Katiya hizo, tani 1,955,763.76 ni mazao ya chakula, huku tani 96,685.33 zikiwa nimazao ya biashara. Kwa makadirio ya mahitaji ya chakula Mkoa unahitaji tani470,000, ambapo kuna ziada ya tani 1,485,763.76.
AfisaKilimo wa Mkoa wa Ruvuma, Onesmo Ngao, amesema kuwa kwa msimu wa kilimo wamwaka 2024/25, mkoa huo umelenga kulima jumla ya hekta 1,379,036 za mazaombalimbali. Hekta 998,745 zitatumika kwa kilimo cha mazao ya chakula,yakitarajiwa kuzalisha tani 1,842,503.
Kwaupande wa mazao ya biashara, mkoa umepanga kulima hekta 363,055, zenyematarajio ya mavuno ya tani 101,252. Aidha, sekta ya mazao ya bustani piaimepewa kipaumbele ambapo hekta 17,236 zitalimwa, huku mavuno yakitarajiwakufikia tani 214,949.
Hatuahizi ni sehemu ya mkakati wa Mkoa wa Ruvuma kuimarisha uzalishaji wa mazao ilikuendelea kuwa na ziada ya chakula, kuchochea uchumi wa wakulima, na kuongezamapato ya mkoa kupitia mazao ya biashara na bustani.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.