Mkoa wa Ruvuma kwa upande wa Lishe bora imekuwa ni changamoto kwa wananchi kutowekea kipaumbele na uelewa mdogo katika ngazi ya familia na Halmashauri.
Akisoma taarifa ya lishe ya Mkoa wa Ruvuma kwenye kikao cha tathimini ya lishe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Isabela Chilumba amesema Mkoa wa Ruvuma una asilimia 41 ya lishe ambayo bado ni ya chini kulingana na hali ya uchumi wa kati wa nchi ya Tanzania tuliyofikia.
Amesema Serikali kwa kutambua umuhimu na kutambua afua za lishe nchini imetoa msukumo zaidi kwa kuimarisha afya ilisainisha mkataba wa utekelezaji wa afua za Lishe kati ya waheshimiwa wa mikoa wote Tanzania bara tarehe 19 Disemba 2017,Wziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanza kutekelezwa Januari 2018.
Hata hivyo amesema utekeleza wa viashiria vya Mkataba umekuwa hautekelezwi kwa ufanisi kwa Mkoa wa Ruvuma kama ilivyopangwa Mkoa uliamua kupeleka nguvu ya kupambana na utapiamlo katika ngazi ya jamii,Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa walisainishana mkataba wa Lishe na Mafisa watendaji Kata ambao nao walisainishana na watendaji wa Vijiji.
‘’Mkoa unatakiwa kufanya Tathimini mara mbili kwa mwaka ,kila baada ya miezi sita, aidha kwa ngazi ya Taifa ya Ofisi ya Rais TAMISEMI Tathimini hiyo itafanyika mara moja kwa mwaka na Halmashauri zote zinatakiwa kufanya Tathmini kila robo mwaka na kuwasilisha taarifa ngazi ya Mkoa’’,alisema Chilumba.
Hata hivyo amesema Halmashauri ni kitovu cha utekelezaji wa afua za Lishe katika Mkoa na kwamba katika kukabiliana na utapia mlo kuwe na mikakati au rasilimali watu na fedha zitengwe kila Halmashauri kwenye bajeti kutoka kwenye vyanzo vya mapato kwa ajili ya kuboresha lishe kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano.
Ameagiza kila mdau wa Lishe katika mkoa aoneshe mchango wake bayana katika kukabiliana na utapia mlo katika eneo analofanyia kazi na kuonesha mbinu ya kukabiliana na tatizo hilo ili kuwezesha hatua stahiki kuchukuliwa.
Imeandikwa na Anet Ndonde
Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Julai 27,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.