Mkoa wa Ruvuma wafikia asilimia 97.34 ya lengo la kuhesabu kaya 450,000 katika zoezi la sensa ya watu 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema hadi kufikia Agosti 28 saa moja jioni Mkoa ulikuwa umehesabu zaidi ya kaya 438,000.
Hata hivyo amesema kazi kubwa ya kuhesabu watu imekamilika na kwamba kinachoendelea hivi sasa ni kukamilisha kuhesabu kaya zilizosahaulika.
“Tunatarajia kutoa taarifa kamili ya sensa Mkoa mzima baada ya kupata taarifa kamili kutoka Wilaya zote”,alisisitiza Kanali Thomas.
Zoezi la sensa ya watu lilianza nchini kote Agosti 23 na kukamilika Agosti 29 mwaka huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.