• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma wapokea watalii zaidi ya 10,000

Imewekwa kuanzia tarehe: September 23rd, 2023

Mkoa wa Ruvuma umepokea jumla ya watalii 10,069  ambao wametembelea vivutio mbalimbali katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas wakati anazungumza kwenye uzinduzi wa Mkakati wa Utalii Mkoa wa Ruvuma kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea,

Akizungumza kwenye uzinduzi huo ulioshirikisha wadau kutoka Halmashauri na wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma na wawakilishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii,WWF,GIZ na PALM, Kanali Thomas amesema kati ya watalii hao watalii wa ndani walikuwa ni 10,027 na watalii kutoka nje ya nchi ni 69.

“Kwa takwimu hizi kama Mkoa tunahitaji kuongeza juhudi zaidi katika kutangaza vivutio vyetu na kuendelea kuhamaisha zaidi  watalii kufika na kutembelea vivutio vyetu’’,alisisitiza Kanali Thomas.

Hata hivyo amesema watalii wengi wanaotoka nje  na kutembelea vivutio vya Mkoa wa Ruvuma wanatoka nchi za Zambia,Malawi,Msumbiji,Zimbabwe na Afrika ya Kusini ambapo amesema juhudi ya kutangaza vivutio ikifanyika Mkoa unaweza kupata watalii wengi kutoka nchi za SADC.

Ameyataja malengo ya kuandaa Mkakati wa Utalii katika Mkoa kuwa ni Pamoja na kuitangaza sekta ya utalii,kuongeza uwajibikaji wa kutunza maliasili zilizopo na kuboresha Maisha ya jamii kwa jumla.

Amezitaja nguzo tatu zilizopo katika mkakati huo kuwa ni kuimarisha utendaji kazi wa kitaasisi kwa kushirikiana,kuendeleza utalii unaohusisha utalii wa kihistoria na kiutamaduni  na kuwezesha mazingira rafiki ya kuendeleza utalii kwa kuimarisha miundombinu ya usafiri na mawasiliano.

Akizungumza kwa niaba ya  wabunge wa Mkoa wa Ruvuma,Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stella Manyanya  ameupongeza Mkoa kuzindua mkakati wa Utalii kwa kuwa uhifadhi na utalii ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Mkoa.

Ametoa rai wananchi kushirikishwa kikamilifu kwenye mkakati wa utalii wa Mkoa ili nao wawe sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo kwa kuwa wanahusika moja kwa moja kwenye utalii.

Miongoni mwa vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Ruvuma ni Pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Nyerere iliyopo wilayani Namtumbo,Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Mwambesi iliyopo wilayani Tunduru,Ziwa Nyasa,Bustani ya wanyamapori ya Ruhila,Makumbusho ya Taifa ya Majimaji,Jiwe la Mbuji na Pori la Akiba Liparamba.

Sekta ya Utalii huchangia zaidi ya asilimia 17 katika Pato la Taifa,pia sekta hiyo imeweza kuchangia ajira za moja kwa moja takriban milioni 1.6.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.