• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma waridhia kupandisha hadhi hifadhi mbili za misitu ya asili

Imewekwa kuanzia tarehe: June 9th, 2021

MKOA wa Ruvuma umeridhia kupandisha hadhi Hifadhi mbili za misitu kuwa mapori ya akiba (Game Reserve) kwa lengo la kuboresha sekta ya utalii kusini.

Mshauri wa Maliasili na Utalii Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe ameyataja mapori hayo kuwa ni Gesimasowa lenye ukubwa wa kilometa za mraba 764 lililopo Halmashauri ya Madaba wilayani Songea na pori la Litumbandyosi lenye ukubwa wa kilometa za mraba 494 lililopo wilayani Mbinga.

“Mapori yote mawili ni sehemu ya ekolojia ya ushoroba wa Selous-Niassa,hata hivyo hadi sasa bado hifadhi  hizo haziajapata Tangazo rasmi la serikali la kuwa ni mapori ya akiba,ingawa mchakato wa kutangaza upo katika hatua za mwisho’’,alisisitiza.

Challe amesema Mkoa wa Ruvuma,una mpango wa kuanzisha mashamba ya wanyapori katika Jumuiya zote tano za uhifadhi,kikiwemo kisiwa cha Lundo ndani ya ziwa Nyasa na katika chuo cha Maliasili cha Likuyusekamaganga wilayani Namtumbo ili wananchi wajifunze na kuanzisha mashamba binafsi ya wanyamapori.

Akizungumzia fursa za utalii zilizopo katika Mkoa wa Ruvuma,amesema Mkoa una fursa za utalii wa kiutamaduni na kiikolojia ambapo amezitaja baadhi ya fursa hizo kuwa ni mapori ya akiba ya Selous,Mwambesi,ziwa Nyasa lenye samaki wa mapambo,visiwa,fukwe za kuvutia na vuvutio vingine lukuki.

Fursa nyingine amezitaja kuwa ni mto Ruvuma wenye maporomoko ya Nakatuta,Tulila na Sunda ambayo yamekuwa yanavutia watalii wengi wa ndani na nje ya nchi.

Challe amezitaja fursa za utalii wa kiutamaduni kuwa ni majengo ya kihistoria yakiwemo makanisa makongwe ya Peramiho,Lituhi na Lundu, makumbusho ya vita ya Majimaji,historia ya machifu wa kiyao,wangoni na historia ya biashara ya utumwa.

Fursa nyingine za utalii wa kiutamaduni amezitaja kuwa ni historia ya wapigania uhuru  wa Afrika,jiwe la Mbuji,mapango ya wamatengo na pango la mlima Chandamali ambalo lilikuwa maficho ya Nduna Songea Mbano wakati wa Vita ya Majimaji.

Ili kuhakikisha vivutio vilivyopo vinaleta tija,Challe amesema Mkoa umeendelea kufanya jitihada za kuboresha miundombinu na matangazo katika vyombo vya habari ambayo yatawezesha fursa hizo kufahamika kitaifa na kimataifa.Ameipongeza serikali kuu kwa kuboresha miundombinu ya barabara na anga hivyo kuvutia watalii na kuufungua Mkoa na ukanda wa kusini katika sekta ya utalii na uwekezaji.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Juni 9,2021

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.