• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKOA wa Ruvuma watoa vitambulisho vya wajasirimali wadogo 72,000

Imewekwa kuanzia tarehe: October 26th, 2020

MKOA wa Ruvuma umefanikiwa kutoa vitambulisho kwa wajasirimali wadogo 59,279 mwaka 2019 na vitambulisho 13,827 vimetolewa kwa wajasirimali wadogo hadi kufikia Oktoba 23 mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme wakati anafungua mkutano wa Baraza Maalum la Biashara  la Mkoa wa Ruvuma kwenye ukumbi wa Herritage Cottage mjini Songea.

Amesema Mkoa umejikita kuhakikisha kuwa malengo ya serikali ya kuwa na uchumi wa viwanda yanafanikiwa ambapo hadi kufikia Juni 2020 Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na jumla ya viwanda 3,485.

Kwa mujibu wa Mndeme kati ya viwanda hivyo,viwanda vikubwa sita,viwanda vya kati 25,viwanda vidogo 190 na viwanda vidogo sana 3,264 na kwamba utekelezaji huo unaendelea kufanywa na sekta binafsi na sekta ya umma.

“Ili kukuza sekta ya Viwanda,Mkoa wa Ruvuma umeendelea kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo,ambapo  Julai 25,2020 Mkoa uliandaa maonesho ya viwanda na uwekezaji kwa lengo la kutangaza fursa zilizopo’’,alisema Mndeme.

Amesema katika kongamano hilo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizindua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa na kwamba Mwongozo huo umesambazwa kwenye Taasisi mbalimbali ambapo hadi sasa wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza ni 22.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa  la Biashara(TNBC) Emanuel Alphance amelitaja lengo la kufanyika Baraza hilo la biashara ni  kufanya tathmini ya mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na kuangalia mikakati na vipaumbele kwa upande wa sekta binafsi na umma katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mwakilishi huyo wa TNBC amesema mfumo huo wa majadiliano kupitia mabaraza ya Taifa,mikoa  na wilaya,unatokana na serikali kuwezesha sekta zote kushiriki katika mipango ya serikali,sanjari na uwepo wa mazingira bora ya kufanya biashara.

Amesema Mabaraza ya biashara yameanzishwa rasmi kwa waraka namba moja wa Rais wa mwaka 2001 na kufuatiwa na azimio la kuanzisha mabaraza ya biashara ya mikoa na wilaya kati ya mwaka 2005 hadi 2008.

Kwa upande wake Yohana Nchimbi ambaye ni Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Ruvuma,amesema TCCIA kama sekta binfasi imenufaika kuanzia wafanyabiashara wa ngazi ya chini hadi juu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ya serikali ya Awamu ya Tano.

“Kwa jitihada kubwa za serikali ya awamu ya Tano,hatuna sababu ya kutokutambua mafanikio haya,hatuwezi kufumba macho tukasema eti hatuyaoni, hatuyasikii, hatunufaiki nayo,wafanyabiashara walioshiriki katika Baraza hilo watakuwa mashahidi wakubwa walionufaika’’,alisisitiza Nchimbi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Masoko Songea(UWABIMASO)  amempongeza Rais Magufuli kwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo vitambulisho ambavyo vimeondoa usumbufu mkubwa waliokuwa wanakabiliwa nao.

Amesema kwa mwaka wafanyabiashara wadogo walikuwa wanalipa ushuru wa zaidi ya shilingi 150,000  ambapo hivi sasa baada ya kupata vitambulisho kwa shilingi 20,000, wafanyabiashara wameweza kutunza fedha zao na kufanya biashara bila usumbufu wowote.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Oktoba 26,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.