MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas amefanya kikao cha kujadili Maendeleo ya Elimu na Maafisa Elimu,Walimu wakuu wa sekondari Mkoa.
Akizungumza katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa amewaasa walimu kuwa na upendo wa dhati wa kukaa na kutenga mda wa kuzungumza changamoto zao binafsi na kuzifikisha katika uongozi husika.
“Hata yale mliyowasilisha kwa Mwenyekiti wenu sijaona changamoto binafsiisipokuwa pesa za uhamisho,lakini Serikali ya Rais Samia inajitahidi sana kulipa madeni ya Walimu”.
Hata hivyoMkuu wa Mkoa amesema changamoto ya walimu kuhamishwa bila utaratibu pamoja na kujiona wengine wanamamlaka.
“Jana nimetoa maelekezo kwa wakurugenzi wasitoe Uhamisho kama hakuna sababu ya msingi na akitoa ahakikishe anamlipa baada ya kulundika madeni kila wakati”.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa Walimu kuzingatia mavazi wawapo katika eneo la Shule ili wanafunzi waweze kufuata mfano mzuri kwa ufaaji wa walimu wao.
“ mimi smati niliiga kutoa kwa Mkuu wangu wa Shule Otieno,alikwa anatuambia ukiitwa sehemu lazima ujue unavaa mavazi ya aina gani unakuta mwalimu kapiga dela na ndala, mwanaume kapiga suluari kamatia chini, mwanafunzi anajifunza nini au tisheti za chama cha walimu tangia mwaka 1191”.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewaasa walimu kuangalia maendeleo binafsi kuwa baada ya mda kuna kustaafu hivyo wahakikishe wanaandaa maisha na wakumbuke wanafamilia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.