Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amempongeza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbinga ,Mbunge,Madiwani, pamoja na wataalamu wa Halmashauri kwa kupata hati safi kwa miaka miwili mfululizo.
Ametoa pongezi hizo wakati anafungua kikao maalum cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mbinga cha kujadili hoja na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
‘’Napenda niwakumbushe kuwa kupata Hati safi kwa miaka miwili mfuulizo kwa kipindi cha 2017/2018 na 2018/2019 siyo jambo dogo ni jambo kubwa sana 2016/2017 mlituletea fedhea kwa kupata hati yenye shaka ambayo haikuzoeleka hapo awali lakini mmehakikisha Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mnairejesha katika viwango vyake vya kupata hati safi hongereni sana’’ alisema mndeme.
Aidha Mndeme alitoa maagizo kuzuia kuwepo kwa hoja za aina moja ,Watendaji wa Halmashauri waendelee kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wakaguzi na Wakuu wa idara washiriki ipasavyo katika kuandaa majibu ya hoja na utekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu.
Hata hivyo Mndeme aliagiza taarifa za hesabu za mwisho wa Mwaka (Annual Financial Statements), kuandaliwa kwa kuzingatia matakwa ya viwango vya kihasibu vya kimataifa katika sekta ya umma(IPSAS). Na kudhibiti upotevu wa mapato katika Halmashauri na vyanzo vya upotevu vithibitiwe kwa kuchukua hatua stahiki.
Mndeme ametoa maagizo kwa Katibu Tawala wa Mkoa kusimamia Fedha na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashaur na ,Kushughuikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za serikali yaliyoainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali.
IMEANDIKWA NA ANET NDONDE
OFISI YA HABARI YA MKUU WA MKOA WA RUVUMA
JUNI 2,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.