• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma akabidhi gari la wagonjwa la kituo cha afya Mapera

Imewekwa kuanzia tarehe: June 16th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma akabidhi gari la wagonjwa la kituo cha afya Mapera

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amekabidhi gari la kisasa la kubebea wagonjwa (Ambulance)  la Kituo  cha Afya  Mapera Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ambalo limenunuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni  138.

Akitoa taarifa kabla ya uzinduzi na makabidhiano ya gari hilo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Juma Mnwele amesema wamefanikiwa kununua gari hilo kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

Amesema gari hilo la wagonjwa limekatiwa Bima kubwa (Premium) ya sh.milioni 6.3 na kwamba limepangiwa kutoa huduma za rufaa kwa wanawake,watoto na wagonjwa wengine katika kituo cha Afya Mapera ambacho kimejengwa kwa fedha za serikali kiasi cha shilingi milioni 400.

“Sisi watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga,tunaona fahari na faraja kuungana na Mhe.Rais John Magufuli ambaye alituletea milioni 400 za kujenga kituo cha afya Mapera na Halmashauri tumenunua gari la wagonjwa ,yawezekana haijawahi kufanyika mahala pengine’’,alisema Mnwele.

Akizungumza kabla ya uzinduzi na kukabidhi gari hilo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewapongeza Halmashauri ya Mbinga kwa kuweza kununua gari la wagonjwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

Amesema Kituo cha afya Mapera ni kati ya vituo vya afya 16 vipya ambavyo vinajengwa katika Mkoa wa Ruvuma kutokana na fedha ambazo zimetolewa na Rais John Magufuli kwa lengo la kuboresha afya kwa wananchi wake.

Hata hivyo Mndeme amesema katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma ujenzi wa hospitali nne za wilaya unaendelea kutekelezwa na kwamba serikali imedhamiria kuona Taifa na wananchi wanakuwa na afya bora ili waweze kutekeleza majukumu yao.

“Ninyi wananchi wa Mbinga kwa namna ya kipekee mmeamua kutumia fedha zenu za mapato ya ndani kununua ambulance ili kumuunga mkono Mhe.Rais wetu katika juhudi  za kuboresha sekta ya afya kwa wananchi’’,alisisitiza.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ameziagiza Halmashauri nyingine mkoani humo kuiga mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kutumia fedha za mapato ya ndani kununua ambulance kwa wale ambao hawana ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa magari ya wagonjwa.

Serikali imeajiri madaktari wapya 24 katika Mkoa wa Ruvuma ambao wamepangiwa kufanya kazi katika  vituo vya afya na hospitali,ikiwemo madaktari wawili ambao wamepangiwa katika kituo cha afya Mapera.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Juni 16,2020 

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.