Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amelaani vikali kitendo cha baadhi ya wananchi wa Matemanga wilaya ya Tunduru kuharibu Miundombinu ya Maji ambayo serikali imetumia mabilioni ya fedha kutekeleza mkiradi hiyo.
Mndeme akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika kijiji cha Matemanga wilaya ya Tunduru alikuta mabomba yameharibiwa na maji kumwagika hovyo huku wananchi wakishindwa kujitolea kufanya matengenezo ya kununua koki.
Mndeme amemwagiza Mwenyekiti wa Kijiji hicho kurekebisha mabomba hayo kwa muda wa siku moja,ambapo ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata wanahusika katika uharibifu wa mabomba hayo.
,,kanga mnanunua kwa shilingi ngapi?au dela mnanunua kwa shilingi ngapi kwa nini mmeshindwa kurekebisha mpaka Mkuu wa Mkoa aje? Rais Alifika hapa mkamuomba akawajengea mradi wa maji halafu mnaharibu maji kwa nini?koki imeharibika meshindwa kurekebisha?.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema wanaotakiwa kulinda miundombinu hiyo ni jumuiya ya wananchi wanaotumia maji ni kwa sababu tanki linajaza maji lita laki moja na serikali inatumia gharama nyingi kujaza maji.
Naye Meneja wa RUWASA Tunduru Mhandisi Primmy Damas amesema Mradi wa Maji Milonde unahusisha upanuzi wa Mradi wa Maji wa Matemanga,mradi huo umegharamiwa na Serikali kuu kupitia Wizara ya Maji na kutekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA)Tunduru kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji na Kata pamoja na wananchi walioweza kuchangia nguvu kazi kwa zaidi ya milioni 215.
Damasi ameitaja Miundombinu ya Mradi huu kuwa inajumuisha vijiji vinne ambavyo vinanufaika na Maji hayo,Matemanga,Milonde,Changalawe,na jaribuni Jumuiya ya watumia maji iliyoundwa na kusajiliwa kwa Mujibu wa sheria Mpya ya Maji namba 5 ya mwaka 2019.
Mradi huu wa Maji Wilaya ya Tunduru ambao umetengewa zaidi ya shilingi 215 hadi sasa milioni 44.5 zimetumika mpaka sasa mradi, utakapokamilika utahudumia jumla ya wakazi 3,600.
Mwandishi ni Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari MKoa wa Ruvuma
26/Juni/2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.