SERIKALI imetoa shilingi billioni 323.4 kukamilisha ujenzi wa barabara ya Namtumbo hadi Tunduru Mangaka yenye urefu wa kilomita 324.6 kwa kiwango cha lami.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge wakati anataja mafanikio ya mwaka mmoja wa serikali ya Awamu ya Sita mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Songea.
Amesema Serikali imetoa pesa kiasi cha Bilioni 129.3 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa barabara ya Mbinga hadi Mbambabay yenye urefu wa kilomita 66 kwa kiwango cha lami.
‘’Niwajulishe pia wananchi wa Mkoa wa Ruvuma Mkoa umepokea jumla ya shilingi Bilioni 14,164,104,629.07 kutoka mfuko wa barabara na Tozo kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami mjini, madaraja 28, makalvati 161, matengenezo ya kawaida km 361.52, muda maalumu km 172.11 na maeneo korofi km 108.4’’, amesema RC Ibuge.
RC Ibuge amesema kukamilika kwa ujenzi wa daraja la mto Ruhuhu lenye urefu wa mita 98.01 limegharimu shilingi Bilioni 6.172 ambalo linaungani Mkoa wa Ruvuma na maeneo yake yote yaweze kufikiwa kwa urahisi.
Hata hivyo amesema kiasi cha fedha Bilioni 37.09 zimetumika kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa kiwanja cha Ndege Songea mjini.
Amesema kiasi cha shilingi Bilioni 6.57 zimetumika kukamilisha ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi katika Manispaa ya Songea.
Akizungumza katika kikao hicho RC Ibuge ameongeza kuwa ujenzi wa bandari mpya ya Ndumbi katika wilaya ya Nyasa unaendelea kwa gharama ya shilingi Bilioni 12.28.
Tutaendelea kuwaletea mafanikio ya mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya sita katika Mkoa wa Ruvuma yaliyotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika habari zinazofuatia kupitia tovuti yetu.
Imeandaliwa na Bahati Nyoni
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Machi 30 2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.