Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas anatarajia kuanza ziara ya siku tatu katika wilaya za Mbinga,Nyasa na Songea kwa lengo la kutembelea miradi ya maliasili na utalii.
Ziara hiyo inatarajia kuanza Septemba 27 na kukamilika Septemba 30 ambapo siku ya kwanza ya ziara yake RC Thomas ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Mtua wilayani Mbinga.
Kulingana na ratiba ya ziara hiyo,Septemba 27,RC Thomas pia atampokea Mwekezaji wa Pori la Akiba Liparamba,kukagua mradi wa ujenzi wa daraja ndani ya hifadhi ya Liparamba na kuweka jiwe la msingi mradi wa nyumba za watumishi wa shamba la miti Mpepo.
Septemba 28 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma atawakabidhi hifadhi ya wanyamapori ya Mbambabay Mamlaka ya wanyamapori Tanzania TAWA na kuzindua uwekezaji wanyamapori katika kisiwa cha Lundo ziwa Nyasa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma anatarajia kukamilisha ziara yake Septemba 30 mwaka huu kwa kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa Wakala wa Misitu Tanzania TFS katika Kijiji cha Wino kwenye safu ya Ifinga,kuzindua mradi wa maji Kijiji cha Ifinga na kuzindua choo cha kisasa katika shule ya msingi Ifinga.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ruvuma
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.