Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe. Aziza Mangosongo amezindua kampeni ya usafi ya wiki moja yenye lengo la kuifanya Mbinga kuwa safi na yenye mvuto zaidi machoni pa watu.
Uzinduzi wa kampeni itakayotamatishwa Septemba 10, ulifanywa katika maeneo ya Soko la Mtumba, Soko Kuu, Stendi kuu, Manzese, Machinjio na Viunga vya bustani vilivyopo barabara kuu ya Songea- Mbamba Bay.
"Kama unadhani kampeni hii inayokwenda kwa jina la ‘Mangosongo Oparesheni Safisha Mji: Mbinga ing’ae’, itaishia kwenye maeneo hayo, unakosea sana",alisisitiza Magasongo
Kampeni iliyobuniwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya itagusa kata zote za Wilaya ya Mbinga na viunga vyake na pia zoezi la usafi litakuwa endelevu.
Akizindua kampeni hiyo Mhe. Aziza aliwataka watendaji wa kata na mitaa kufanya kazi kwa bidii bila kusukumwa ili kuhakikisha kampeni hiyo inafanikisha suala zima la usafi
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.