MKUU wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma mh.Filberto Sanga amewataka wananchi,na viongozi wote Wilayani Nyasa kukamilisha Ujenzi wa miradi kabla ya tarehe 30/09/2023.
Agizo hili amelitoa katika Ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo katika kata ya Chiwanda, Mtipwili na KilosaTarafa ya Ruhekei Wilayani Nyasa.
MH.Sanga amefafanua kuwa lengo la kufanya Ziara hiyo ni kujionea jinsi miradi inyoendelea kutekelezwa katika maeneo hayo.
"Ninawaagiza miradi hii iwe imekamilika kabla ya tarehe 30/09/2023, Kwa kuwa fedha hizi zimeletwa na MH.Rais SAMIA Suluhu Hassan Kwa ajili ya kutatua kero Za wananchi,hivyo Kila kiongoz, wananchi wahakikishe miradi yote inakamilika Kwa muda uliopangwa"
Miradi aliyoitembelea ni madarasa 3 ya shule ya msingi Chiwindi,Bweni la wasichana shule ya Sekondari Nyasa,(Kata ya Chiwanda) Matundu ya vyoo shule ya msingi Mtipwili,Kata ya Mtipwili) madarasa 3 ya shule ya msingi Nangombo, Ujenzi wa shule mpya ya Kilosa na Ujenzi wa Bwalo la chakula shule ya Sekondari ya limbo (kata ya Kilosa)
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.