• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MKUU wa Wilaya ya Nyasa akabidhi cheti za usajiri chama kipya cha msingi cha Ushirika

Imewekwa kuanzia tarehe: September 5th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi  Isabela Chilumba, jana amekabidhi Cheti cha Usajili wa Chama Kipya cha Msingi cha Ushirika wa Mazao Litindo,  ambacho kimesogeza karibu  Huduma ya kuuza mazao kwa wakulima wa Kijiji cha Litindo kata ya Luhangarasi Wilayani Nyasa, Makabidhiano  yaliyofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Serikali ya kijiji  cha Litindo Wilayani hapa.

Akikabidhi Cheti Cha Usajili amewataka wananchi wa Kijiji hicho, na Wilaya ya Nyasa kwa ujumla, hususani Vijana,  kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa, kwa kuwa Ardhi  ipo ya kutosha inayostawisha zao la kahawa ili kuongeza kipato Ngazi ya kaya na Taifa kwa ujumla.

Chilumba alifafanua kuwa,  wananchi wa kijiji cha Litindo wamefurahia kupewa Cheti cha Usajili wa Chama Cha Ushirika cha Msingi, ambacho ilikuwa ni  kero ya wananchi wa kijiji hicho kwa kuwa, awali walikuwa wanasafirisha mazao yao umbali mrefu, na walikuwa wakiuza Kwenye Chama cha Luhangarasi Amcos, lakini kwa sasa watakuwa wanauza katika Chama chao ambacho kimepata usajili.

Aliongeza kuwa, wasifurahie kupata usajili tu peke yake bali waongeze uzalishaji wa zao hilo, kwa kuongeza mashamba mapya na kupanda mbegu bora za kisasa, ambazo huzalisha mazao mengi na kwa muda mfupi. Badala ya kusubiri mashamba ya kurithi peke yake. Amewaagiza Watendaji wa Kata na Kijiji kuhakikisha kila mkulima anaongeza Uzalishaji wa zao la Kahawa kwa kila Msimu wa kilimo.

“Ndugu wakulima nimewaona leo mnafurahia kupewa cheti cha Usajili wa Chama chenu, lakini furaha hiyo isiishie hapa bali iwe fursa kwenu ya kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa hapa kijini kwenu na Wilaya ya Nyasa kwa ujumla, hasa vijana kila kijana anatakiwa kuwa na walao hekari mbili kwa kufanya hivi hata chama chenu cha ushirika kitakuwa na nguvu kwa kuwa kitakuwa na mazao mengi”.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wa chama hicho kuwa waaminifu na waadilifu katika kutekeleza majukumu yao kwa kulinda na kutunza Fedha na mali ya Chama ili wananchi wakipende Chama chao, na kuongeza uzalishaji wa zao hilo. Pia aliwatahadharisha kuwa Serikali Wilayani hapa ipo makini na itawachukulia hatua za kisheria Viongozi wa Vyama vya Ushirika watakaohusika na Wizi au upotevu wa Fedha za wakulima.

Kwa upande wao wanachama na wakulima wa mazao Katika Kijiji hicho wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Nyasa kwa uchapakazi wake na kutatua Changamoto mbalimbali za Wananchi kwa haraka, na kumwomba aendelee kuwasaidia na kuwaongoza ili wazidi kupata  maendeleo, na kusema kuwa wataendelea kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kuwa changamoto iliyokuwa inawakabili imetatuliwa.

IMEANDALIWA NA

NETHO SICHALI

AFISA HABARI NYASA DC

0767417197

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.