Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Pololet Mgema amewetaka viongozi wa mitaa katika wilaya ya Songea kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa ifikapo siku hiyo ya Sensa
Ameyasema hayo katika ukumbi wa manispaa ya Songea mjini alipokutana na wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji amewaomba na kuwataka watimize wajibu wao wa kuwaongoza makarani kwani serikali imetumia fedha nyingi kwenye zoezi hili la Sensa
“Wenyeviti wezangu pamoja na watendaji tutangulize uzalendo na uaminifu itatufanya kuweza kukumbuka zoezi lililopo mbele yetu sisi ni viongozi wa watu kwahiyo nawaomba sana jambo hili tulichukulie kwa uzito unaostahili twendeni mkawaongoze makarani na kushirikiana nao bega kwa bega” alisema Mgema
Mgema ameyasema hayo huku zikiwa zimebakia siku mbili kutimia siku ya zoezi la Sensa ya watu na makazi ambayo itafanyika Agosti tarehe 23 ambapo itakuwa siku ya jumanne
Naye Juma Nindi Mwenyekiti wa Mtaa wa Luhira seko kwaniaba ya wenyekiti wezake amesema wapo atayari kwa kushirikiana na kuwaongoza makarani kwani nizoezi muhimu kwa taifa na ambalo ufanyika baada ya miaka 10
Sensa ya watu na makazi inatarajia kufanyika nchini kote Agosti 23 mwaka huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.