KIONGOZI wa Mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru Lt Josephine Mwambashi ameweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mbinga Vijijini na Mradi wa Maji wa maboresho ya Huduma ya Maji Mbinga Mjini.
Akitoa taarifa hiyo kabla ya kuweka Jiwe la msingi Dr. Louis Chomboko amesema Serikali imeleta kiasi cha shiringi milioni miatano kwaajili ya ujenzi wa majengo matatu ya awali likiwemo jengo la wagonjwa wan je(OPD)jengo la maabara na kichomeo Taka.
Dr. Chomboko ameelezea lengo la ujenzi wa Hospitali hiyo ni kuboresha huduma za afya ya jamii ikiwemo wakazi 300,000 kutoka Kata za Halmashauri hiyo pamoja na maeneo ya Karibu kama Songea, Shughuli za ujenzi zilianza Juni 1,2021 na kutarajia kukamilika Septemba 30,2021 .M
“Hadi kufikia hatua hii kiasi cha zaidi ya shilingi milioni miatatu zimetumika na Fedha ya serikali imetumika kiasi cha zaidi ya shilingi milioni miambili themanini kwaajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi”.
Kwa upande wake Meneja ufundi mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Songea Jafari Yahaya amesema walipokea maelekezo kutoka Wizara ya Maji ya utekelezaji wa mradi wa maboresho ya huduma ya maji Mbinga Mjini .
Yahaya ameelezea lengo la mradi huo ni kusogeza Huduma ya maji karibu na wananchi na kuwapunguzia umbali mrefu wa kutafuta maji ili waweze kushiriki katika shughuli za maendeleo na kutekeleza kauli mbiu ya “kumtua mama ndoo kichwani”.
Amesema Mradi huo umegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja ambapo Wizara ya Fedha imetoa zaidi ya shilingi milioni miatano ili kutekeleza mradi huo , na kufikia asilimia 75 hadi sasa na kuhudumia wakazi wa Mbinga wapatao 12,000.
Kiongozi wa mbio za Mwenge Lt Mwambasi kabla ya kuweka jiwe la msingi alibaini wananchi hawakushirikishwa juu ya ujenzi wa mradi huo hivyo ameagiza uongozi wa Wilaya kutoa taarifa kwa wananchi kupitia vikao vya kisheria.
https://www.youtube.com/watch?v=Ca16mT-cX2s
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 4,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.