Mradi wa ujenzi wa bandari ya Mbambabay katika Ziwa Nyasa, wilayani Nyasa mkoani Ruvuma, unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 26, 2026, na unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100.
Mradi huu, wenye thamani ya bilioni 81, ulianza tarehe 27 Januari 2024, na unajumuisha ujenzi wa gati, majengo, na miundombinu ya zimamoto.
Mwakilishi wa kampuni inayotekeleza ujenzi, Mhandisi Timoth Mliyuka, alisema kwamba bandari hii itasaidia kuimarisha uchumi wa wilaya ya Nyasa na kuunganisha bandari ya Mtwara, ambapo mizigo itapitia kwenda nchi jirani za Zambia na Malawi. Bandari hiyo itakuwa na uwezo wa kupaki meli mbili kwa wakati mmoja.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Starwat Nombo amempongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo na kwamba baadhi ya bidhaa, kama mahindi, zitakuwa zikisafirishwa kwenda Malawi na Msumbiji,kupitia bandari ya Mbambabay.
Amesema mradi huo utakapokamilika, mji wa Mbambabay utafunguka, na fursa za biashara, ajira, na maendeleo zitapatikana kwa vijana na jamii kwa ujumla
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.