• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MSITAFUTE migogoro na vyama vya siasa

Imewekwa kuanzia tarehe: August 8th, 2020

Msitafute migogoro na vyama vya siasa

MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Songea mjini mkoani Ruvuma Tina Sekambo amewatahadharisha wasimamizi  wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata katika Manispaa hiyo kuepuka migogoro na vyama vya siasa kwa  kwa kusimamia mchakato  wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria za Tume ya Uchaguzi.

Sekambo ametoa tahadhari hiyo kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo mjini Songea, wakati anazungumza kabla ya kufungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi kutoka kata zote 21  kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.

 “Tume ya Uchaguzi inasisitiza sana,tusitafute migogoro na vyama vya siasa,tuepuke kabisa migogoro ,uchaguzi  asilimia 100 unaendeshwa na  sheria ,ukikosea hata nukta ni tatizo,tunatakiwa tusome maelekezo yote vizuri ili kufanya mchakato wa uchaguzi mwaka huu kwa ufanisi’’,alisisitiza Sekambo.

Msimamizi huyo wa Uchaguzi Jimbo la Songea mjini pia  amewataka wasimamizi hao wasaidizi siku ya wagombea kuchukua fomu hadi siku ya uteuzi  wanatakiwa kuwepo ofisini muda wote na kwamba siku tatu kabla, wanasiasa wanaruhusiwa kuleta fomu zao na kukaguliwa kubaini iwapo zina makosa au  zipo sahihi.

Amesema Tume ya uchaguzi imeamua kutoa mafunzo hayo ya siku tatu ili kufanikisha zoezi la Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ambapo amewaasa kuhakikisha wanazingatia  mafunzo yote ambayo watapewa na Tume ya Uchaguzi badala ya kufanyakazi kwa mazoea.

“Hakikisheni mnazingatia matakwa ya Katiba,Sheria,Kanuni zinazosimamia Uchaguzi,maadili ya uchaguzi na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na NEC’’,alisisitiza Sekambo.

Kwa upande wake Afisa Uchaguzi Manispaa ya Songea Christopher Ngonyani  amesema mafunzo hayo yameshirikisha wasimamizi wasaidizi  42 kutoka Kata 21 zilizopo katika Manispaa hiyo na kwamba wote walioteuliwa na NEC wamehudhuria mafunzo hayo.

Afisa Uchaguzi huyo amewaasa washiriki wa mafunzo kuzingatia mafunzo wanayopewa  na kuhakikisha kila msimamizi anayatambua maeneo ambayo atafanyia kazi  ikiwemo miundombinu ya kufika katika kata na vituo vya kupigia kura.

Wasimamzi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata Manispaa ya Songea wameapishwa na  Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi  mkoani Ruvuma  Livini Lyakinana

Uchaguzi Mkuu wa Rais,wabunge na madiwani unatarajia kufanyika nchini Oktoba 28 mwaka huu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Agosti 8,2020

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.