• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MSITU wa Matogoro una vivutio vya aina mbalimbali

Imewekwa kuanzia tarehe: January 27th, 2025

Mlima Matogoro ni moja ya vivutio vikubwa vya utalii na urithi wa kihistoria mkoani Ruvuma, hususan katika Manispaa ya Songea. Msitu wa hifadhi ya mazingira asilia wa Matogoro una sifa ya kuwa na mandhari nzuri, bayoanuai tajiri, na historia ya kipekee inayovutia wageni wa ndani na nje ya nchi.

Vivutio vya Mlima Matogoro

Kwa mujibu wa Mhifadhi wa Msitu wa Mazingira Asilia Matogoro, Bw. Mussa Kitivo, msitu huu una vivutio mbalimbali vinavyosaidia kukuza sekta ya utalii mkoani Ruvuma. Baadhi ya vivutio hivyo ni pamoja na:

Mandhari na Maeneo ya Kutazama Mji wa Songea

Mlima Matogoro una miinuko mikubwa inayoleta mwonekano mzuri wa mji wa Songea na vijiji vyake. Kutokea kileleni mwa mlima, wageni wanaweza kufurahia mandhari nzuri ya jiji na mazingira yanayouzunguka.

Chanzo cha Mto Ruvuma


Mto Ruvuma, ambao ni mojawapo ya mito mikubwa nchini Tanzania yenye urefu wa takribani kilomita 800, una chanzo chake ndani ya hifadhi hii. Mto huu husafiri hadi kufikia Bahari ya Hindi mkoani Mtwara, ukiwa tegemeo kubwa la maji kwa jamii na viumbe hai ndani ya Bonde la Ruvuma.


Vyanzo vya Maji Muhimu kwa Manispaa ya Songea


Msitu wa Matogoro una vyanzo vya maji takriban vinane (intake) vinavyotokana na mito ya Ruvuma, Luhira, na Lipasi, ambavyo ni tegemeo kubwa la maji kwa wakazi wa Songea.


Mapango ya Kihistoria


Ndani ya hifadhi hii, kuna mapango yanayotumiwa kwa tiba za jadi na matambiko na wakazi wa Songea na mikoa jirani. Mapango haya yana historia ya kipekee inayohusiana na mila na desturi za wenyeji.


Wanyama na Aina Mbalimbali za Ndege


Msitu wa Matogoro ni makazi ya wanyama mbalimbali wakiwemo swala, digidigi, nyegere, nyani, chui, nyati, na simba kwa baadhi ya nyakati. Aidha, kuna aina mbalimbali za ndege na vipepeo wanaochangia kuvutia watalii na watafiti wa bayoanuai.


Uoto wa Asili na Hali ya Hewa ya Kipekee


Msitu huu una uoto wa asili wa mimea mbalimbali unaosaidia kuhifadhi mazingira na kuwa na hali ya hewa ya kipekee ambayo haipatikani sehemu nyingine ndani ya mkoa wa Ruvuma.


Historia ya Hifadhi ya Msitu wa Matogoro


Msitu wa Matogoro ulitangazwa kuwa msitu wa hifadhi ya serikali kuu kupitia Gazeti la Serikali kwa Tangazo No. 260 la tarehe 06/11/1951 na kupewa JB No. 110. Hifadhi hii ina ukubwa wa jumla ya hekta 7,457.24.


Mnamo mwaka wa fedha 2022/2023, hadhi ya msitu huu ilipandishwa na kuwa Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia wa Matogoro kupitia Tangazo la Serikali No. 7778 la tarehe 30/12/2022. Usimamizi wa hifadhi unafanywa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka eneo hilo.


Mnamo mwaka 1961, Idara ya Misitu na Nyuki ilianzisha upandaji wa miti ya kigeni aina ya misindano (Pinus spp) kwa ajili ya kutoa malighafi za misitu kwa Manispaa ya Songea. Hata hivyo, mwaka 2000, upandaji wa miti ya kigeni ulisitishwa, na kuanza kupandwa miti ya asili ili kulinda vyanzo vya maji.


Maendeleo ya Miundombinu ya Utalii

Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ilipokea jumla ya Tsh 394,135,000 kupitia Mpango wa Maendeleo na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya utalii ndani ya hifadhi. Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na,Ujenzi wa barabara ya vumbi yenye urefu wa km 9,Kuanzisha njia ndogo za matembezi kwa miguu (nature trail) zenye urefu wa km 4.3. Na Kujenga lango la kuingilia katika hifadhi ili kurahisisha upatikanaji wa vivutio.


Ongezeko la Watalii na Mapato


Katika mwaka wa fedha 2023/2024, hifadhi ya Matogoro ilipokea jumla ya watalii wa ndani 2,341 na watalii wa nje 30, na kufanikisha ukusanyaji wa mapato ya Tsh 5,467,000/=.


Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 hadi sasa, hifadhi imekusanya Tsh 1,472,390/=.


Mikakati ya Kuendeleza Utalii katika Hifadhi ya Matogoro

Ili kuboresha na kuongeza mapato yanayotokana na utalii, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeweka mikakati kadhaa, ikiwemo,Kutafuta mwekezaji kwa ajili ya kujenga hoteli ya kitalii katika eneo la “View Point” ambalo linatoa mwonekano mzuri wa mji wa Songea.

Mikakati mingine ni Kutangaza vivutio vya hifadhi ili kuongeza idadi ya watalii kutoka 2,341 wa sasa hadi 5,000 kwa mwaka,Kujenga miundombinu ya kudumu kama vile vyoo vya kisasa, jiko la kisasa, na vifaa vya michezo kwa watoto katika eneo la picnic site na Kufanya utafiti wa mwelekeo wa upepo kwa ajili ya utalii wa kuruka na parachuti (paragliding) kutoka View Point No.2.

Mikakati mingine ni Kuanza kutoa huduma za malazi kwa wageni wanaotaka kulala ndani ya hifadhi kwa kutumia mahema ya hadhi mbalimbali (Ordinary & Executive).

Mlima Matogoro ni hazina muhimu kwa utalii wa mkoa wa Ruvuma. Mandhari yake ya kuvutia, urithi wa kihistoria, na viumbe hai vinavyopatikana ndani ya hifadhi hii vinaifanya kuwa mojawapo ya sehemu bora za kutembelea kwa watalii wa ndani na nje ya nchi. 


Juhudi za kuboresha miundombinu na kuongeza vivutio zinatarajiwa kuleta maendeleo makubwa kwa sekta ya utalii na uchumi wa Manispaa ya Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.