KUELEKEA maadhimisho ya wiki maji inayoanzia Machi 16 hadi 22 mwaka huu ,Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) imesema kwa wateja wa muunganisho mpya,mteja atatakiwa kulipa nusu ya gharama kisha ataunganishwa na huduma ya maji safi.
Mkurugenzi Mtendaji wa SOUWASA Mhandisi Patrick Kibasa amebainsha kuwa deni ambalo litabaki baada ya mteja kuunganishiwa huduma ya maji,litalipwa baada ya makubaliano kati ya mteja na SOUWASA.
Hata hivyo amesema kuanzia Machi 16 hadi Aprili 16 mwaka huu SOUWASA imeondoa gharama za urejeshaji wa huduma ya maji kwa wateja waliositishiwa huduma hiyo.
Kaulimbiu ya wiki ya maji mwaka huu ni kuongeza kasi ya mabadiliko katika sekta ya maji kwa maendeleo ya uchumi endelevu
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.