MWENGE WA UHURU WABISHA HODI NAMTUMBO
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngolo Malenya amesema kuwa Mwenge wa Uhuru unaokimbizwa katika Wilaya hiyo utakagua,utaweka mawe ya msingi na kuzindua miradi kumi ya maendeleo yenye thamani ya sh. Bilioni 2.5
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Tunduru alisema kuwa mwenge huo ukiwa Wilayani Namtumbo utaweka jiwe la msingi kwenye mradi wa barabara ,Mradi wa kituo cha mafuta,mradi wa bweni Veta, ugawaji wa vifaa kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Ameitaja miradi mingine kukagua shughuli za lishe, kuzindua klabu ya kupinga Rushwa, kutembelea mradi wa uhifadhi wa mazingira Luegu, pamoja na kuzindua kisima kilichoboreshwa Kijiji Ruvuma.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.