• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MWENGE wa Uhuru wapitia miradi ya bilioni 2.5 Namtumbo

Imewekwa kuanzia tarehe: June 9th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngolo Malenya amesema kuwa Mwenge wa Uhuru katika Wilaya hiyo umefungua,kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi kumi ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 2.5

Malenya ameitaja miongoni mwa miradi hiyo kuwa ni mradi wa ujenzi wa barabara za lami mjini Namtumbo ambao unagharimu Zaidi ya shilingi milioni 889,mradi ambao unahusisha ujenzi wa  wa barabara kwa kiwango cha changarawe,lami nyepesi,kokoto na uwekaji taa za barabarani 43.

Mradi mwingine ambao umepitiwa na Mwenge wa Uhuru ni ujenzi wa mabweni katika chuo cha Ufundi Stadi VETA Namtumbo,mradi ambao unatarajia kugharimu Zaidi ya shilingi milioni 814.

Mwenge wa Uhuru pia umepitia miradi ya lishe na shamba la miti katika Kijiji cha Luegu ambapo hadi kufikia mwaka 2023 shamba hilo lilikuwa na miti  5480 aina ya mitiki na kwamba mradi huo umegharimu shilingi milioni 45.

Mwenge wa Uhuru pia umepitia mradi wa chemchem ya maji ya asili iliyoboreshwa katika Kijiji cha Ruvuma Kata ya Hanga ambapo Zaidi ya shilingi milioni mbili zimetumika kuboresha chemchem hiyo.

Miradi mingine iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru wilayani Namtumbo ni kituo cha mafuta cha KSM  kilichoanzishwa na Said Kazibure ambapo hadi sasa mradi umegharimu  shilingi milioni 515 na kwamba mradi unatarajia kutoa ajira 25.

Mwenge wa Uhuru umepokea  taarifa ya ugawaji wa vyandarua kwa akinamama wajawazito,makundi maalum na Watoto chini ya mwaka mmoja,pia Mwenge wa uhuru umepokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za ukatili wa kijinsia na watu wenye ulemavu.

Akizungumza baada ya kukagua mradi wa barabara za lami mjini Namtumbo,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godref Mnzava ameipongeza TARURA kwa usimamizi mzuri wa mradi huo ambao pia umezingatia mfumo wa ununuzi wa umma katika utekelezaji wake.

Amesema serikali inaendelea kuelekeza manunuzi yote na zabuni zake yapite kwenye mfumo wa manunuzi wa kidigitali wa NEST  ambapo amewapongeza TARURA kwa kutekeleza agizo hilo kwa kupitisha zabuni kwenye mfumo hivyo kuongeza uwazi na uwajibikaji.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.