• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

MWENGE wa Uhuru watembelea mradi mkubwa wa barabara Songea

Imewekwa kuanzia tarehe: June 15th, 2024

Mwenge wa Uhuru 2024 umetembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara za lami nzito zinazogharimu  Zaidi ya shilingi bilioni 22 katika mji wa Songea mkoani Ruvuma.

Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru,Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Wakili Bashir Muhoja amesema Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 12 zilizobahatika kupata mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara za lami nzito zenye urefu wa kilometa 10.1.

Amebainisha mradi huo una jumla ya barabara 20 za lami katikati ya Mji wa Songea ambazo zitatengezwa kupitia mradi huo ambao umefadhiliwa na  Jumjuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA) kupitia Benki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha miundombinu na ushindani wa miji,Manispaa na Majiji nchini Tanzania (TACTC).

Hata hivyo amebainisha kuwa mradi huo unaratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI na kwamba hadi sasa Mkandarasi amefikia asilimia 20 ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo.

“Ujenzi wa barabara hizi utaleeta manufaa ya kuwa na miundombinu bora na inayopitika wakati wote

hivyo kuwezesha watumiaji wa barabara kupunguza gharama za uendeshaji wa vifaa vya moto,kutoa ajira kwa wananchi 134 na kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuwa barabara hizo zitakuwa na taa’’,alisisitiza.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava ameagiza Mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili uanze kuwahudumia wananchi wa Mji wa Songea.

Mwenge wa Uhuru pia umeweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea ambao unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 500.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava pia amekubali kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa vyumba kumi na matundu kumi  katika shule ya sekondari ta Londoni Manispaa ya Songea,mradi ambao unagharimu Zaidi ya shilingi milioni 259.

Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Manispaa ya Songea umetembelea mradi wa maji Mtaa wa Pambazuko Kata ya Tanga unaogharimu Zaidi ya shilingi milioni 578 wenye uwezo wa kuhudumia wananchi wapata0 15,990.

Mradi huo unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Ustawi wa Mazingira Songea (SOUWASA) kwa kushirikiana na Wizara  ya Mazingira.

Mwenge wa Uhuru pia umepitia taarifa ya mapambano dhidi ya malaria kwa ugawaji wa vyandarua kwa mama wajawazito,makundi maalum na Watoto chini ya mwaka mmoja ambapo hadi sasa vyandarua  vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 356 vimegawiwa bure.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.