Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kelvin Mapunda amewataka machifu wa Wilaya ya Mbinga kuendeleza umoja na mshikamano na kulinda maadili kwa vijana.
Mapunda ametoa wito huo wakati anazungumza na na machifu wa Wilaya ya Mbinga ofisi kwake mjini Mbinga.
“Tutandaa utaratibu mzuri ndani ya Halmashauri ili tuone namna ya kuwaalika kwenye vikao vyetu vya Baraza ili kuwezesha kujenga maadili ya mtanzania kulingana na mil ana desturi zetu," alisisitiza Mapunda.
Ameongeza kuwa kutoa elimu mara kwa mara kupitia Baraza la madiwani kutasaidia kuleta muunganiko wa pamoja hasa pale baadhi ya mambo yanapohitaji busara za wazee.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Bi. Amina Seif amewashukuru wazee hao na kuwaomba wazidishe ushirikiano na Halmashauri hiyo kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.