MWENYEKITI wa Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma Mheshimiwa Teofanes Mlelwa amewapongeza wananchi wa kijiji cha Magingo kata ya Mkongotemba kwa kuanzisha sekondari yao ambayo serikali imetoa fedha za kuendeleza miundombinu ya shule hiyo ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira rafiki/
Mlelwa ametoa pongezi hizo wakati anazungumza kwenye mahafali ya kidato cha nne ambapo pia Mkuu wa shule alizitaja baadhi ya changamoto zilizopo katika shule hiyo kuwa ni upungufu wa mabweni na nyumba za walimu..
Afisa Elimu Sekondari Taaluma wa Halmashauri ya MadabaDevis Mwasi akijibu changamoto hizo amesema wataandika andiko maalumu kupitia bajeti ya mwaka wa Fedha 2024/2025 ili kuondoa changamto za mabweni na nyumba za walimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.