Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Judith Kapinga amezindua kituo cha mauzo ya makaa ya mawe kinachomilikiwa na Kampuni ya Marketing Insight Limited MilCoal kilichopo katika Kijiji cha Paradiso Kata ya Ruanda Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma.
Mhe,Kapinga amesema kuwa Sera ya Nishati na Sera ya Madini zinatambua michango ya Kampuni kwenye maeneo mbalimbali Nchini ili kuhakikisha Wananchi wanaozunguka Kampuni hizo wananufaika nazo.
Katika hatua nyingine Mheshimiwa Judith Kapinga amesema kuwa uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya MILCOAL unasaidia ongezeko la ukuaji wa uchumi pamoja na fursa za ajira nchini.
Hata hivyo amesema kutokana na hitaji la umeme katika mgodi wa MILCOAL Naibu Waziri wa Nishati amesema TANESCO wanatarajia kufikisha umeme hivi karibuni kwa gharama ya shilingi milioni 280.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mheshimiwa Peresi Magiri , akitoa salamu za Mkoa, ameipongeza Kampuni ya MILCOAL pamoja na kampuni mbalimbali zilizopo katika maeneo hayo,pia amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika Mkoa wa Ruvuma.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Ruanda Dougras Mwingira amewapongeza wamiliki wa mgodi huo akisema kuwa kuwepo kwa mradi huo kumeleta fursa kwa Wananchi wa Kijiji hicho kwa kukuza fursa ya uchumi kwa wakazi wa kata hiyo.
Mussa Haji ni Mwakilishi wa Kampuni ya MILCOAL amesema kampuni hiyo imefanikiwa kufanya mauzo ya tani laki 330,000 huku wakichangia kiasi kikubwa katika utoaji wa ajira kwa wakazi wa maeneo jirani na Mgodi huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.