Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngollo Malenya amesema wilaya hiyo inafanya maadhimisho ya siku ya wanawake kiwilaya kwa siku mbili kuanzia Machi 5 hadi 6,2024 ili kutoa fursa kwa wanawake kushiriki shughuli za maendeleo.
Amesema katika siku hizo wanawake watashiriki kufanya usafi wa mazingira,kupanda miti,uchangiaji damu,utoaji wa elimu ya afya na upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi.
Ngollo ameitaja shughuli nyingine itakayofanyika katika maadhimisho hayo ni kutoa taulo za kike kwa kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani humo.
“Katika maadhimisho haya tumepanga kuwatembelea Watoto wenye mahitaji maalum katika kituo cha shule ya msingi Nambehena ambako tutawagawia Watoto hao sare za shule na sabauni’’,alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
Ametoa rai kwa wadau wote wa maendeleo kuungana na wanawake wa Wilaya ya Namtumbo katika siku mbili hizo za kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi 8,2024.
Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani katika Mkoa wa Ruvuma,kimkoa yanatarajia kufanyika wilayani Mbinga siku ya Machi 8,2024.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Wekeza kwa wanawake,kurahakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”.
Kaulimbiu hii inalenga kuhamasisha jamii kuwekeza kwa wanawake ili kuleta usawa wa kijinsia Pamoja na kukumbushana umuhimu wa usawa wa kijinsia katika kuchochea ukuaji wa Uchumi,maendeleo jumuishi na ustawi wa jamii kwa maendeleo endelevu kwa wanawake
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.