katika hali isiyo ya kawaida kwa wilaya ya pembezoni kama Namtumbo iliyopo mkoani Ruvuma upepo wa mabadiliko umeshika kasi baada ya kutangazwa rasmi kwa mradi mkubwa wa uchimbaji wa madini ya Uranium wenye thamani ya dola bilioni 1.2.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mheshimiwa Ngollo Malenya, pichani kulia amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mantra Rosatom, Bw. Alexander Ryabchenko, katika mazungumzo yaliyolenga maandalizi ya uzinduzi rasmi wa mradi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Julai 2025.
Mradi huo si tu kwamba unakuja na mitaji mikubwa kutoka nje, bali pia unatarajiwa kuajiri takribani wafanyakazi 3,600, hivyo kuifanya Namtumbo kuwa kitovu kipya cha ajira na maendeleo ya kiuchumi.
Mheshimiwa Malenya amesema mradi huo ni neema ya kipekee kwa wananchi wa Namtumbo na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
“Natoa rai kwa wana Namtumbo kuunga mkono mradi huu maana utakuwa sehemu ya kukuza uchumi,” alisisitiza.
Ametoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kujiandaa na kujipanga kwa ajili ya fursa mbalimbali zitakazozalishwa na mradi huo, ikiwemo huduma za kijamii, biashara, na ujuzi wa kazi za viwandani.
Huu ni mwanzo wa zama mpya kwa Namtumbo zama ambazo zinaweza kubadili kabisa taswira ya kiuchumi na kijamii ya wilaya hiyo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.