Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma kwa kipindi cha miaka sita 2015/2016 hadi 2020/2021 imekopesha vikundi 229 wenye wanachama zaidi ya 800 jumla ya shilingi milioni 172,500,000.
Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo bwana Peres Kamugisha aliyasema hayo kwenye semina elekezi ya ujasilimali na maendeleo ya biashara kwa vikundi vilivyopatiwa mkopo katika halmashauri hiyo.
Bwana Kamugisha alisema halmashauri imelazimika kutoa semina elekezi kwa vikundi vilivyopatiwa mkopo ili kuwa na uelewa kuhusu namna ya kufanya shughuli za ujasiliamali na kuwa na maendeleo ya kweli katika biashara zao na waweze kulipa mikopo wanayopewa kadiri ya sheria ya mikopo za mwaka 2021.
Alisema zipo changamoto kubwa ya baadhi ya vikundi kutokuwa na uaminifu na kupelekea kutorejesha mikopo kwa wakati licha ya kuwapatia semina elekeza ya ujasiliamali pamoja na namna ya kuendesha biashara zao mara kwa mara.
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume Kizigo alialikwa katika semina hiyo na kuwataka wanufaika ya mikopo ya vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kuzitumia fedha hizo katika malengo yaliyokusudiwa .
Kizigo alidai wapo wanaopata mkopo na hawataki kurudisha hali inayokwamisha vikundi vingine vyenye uhitaji wa kupata mikopo hiyo kukosa kupatiwa mikopo kutokana na baadhi ya vikundi kutokuwa waaminifu wa kurudisha mikopo.
Wapo walemavu wanaowezeshwa kupata mikopo ili wajiinue kimapato lakini wapo wengine wanatumia kigezo hicho cha ulemavu kama kinga ya kutorudisha mikopo na wanaposhindwa kurudisha mikopo wanajizuia kupata mkopo tena .
Aliwataka walemavu kutojiona kuwa wao ni tofauti na makundi mengine bali kuwa wao ni sawa na makundi mengine na wanatakiwa kupata mikopo na kuirudisha ili waendelee kuaminiwa na serikali na kukopeshwa mara kwa mara.
Asha kamtende ni mnufaika wa mkopo kutoka katika kikundi cha wajasiliamali nguvu moja pamoja na kuishukuru serikali kuwajali wajasiliamali wadogo kwa kuwapatia mikopo alisema kikundi chao kimewezeshwa kupata 1,500,000 na wataitumia fedha hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na kasha kurudisha mkopo huo kwa wakati ili serikali iwaamini na kisha kuendelea kukopeshwa mara kwa mara.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo kwa mwaka fedha 2020/2021 hadi mei halmashauri imetoa kiasi cha shilingi 80,000,000 kupitia mapato yake ya ndani kwa vikundi 25 vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu vyenye jumla ya wanachama 60 ambapo kwa miaka sita jumla ya shilingi milioni 172,500,000 zimekopeshwa kwa vikundi vya vijana 94, vyenye wanachama310 vimepatiwa mkopo wa shilingi 168,800,000,vikundi vya watu wenye ulemavu vikundi 26 vyenye wanachama zaidi ya 70 jumla ya shilingi 47,000,000 zilikopeshwa na saccos ya vijana moja jumla ya shilingi 5,350,000.
Imetolewa na Afisa Habari wilaya ya Namtumbo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.