Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia Nape Nauye ameupongeza Mkoa wa Ruvuma kwa kasi ya zoezi la uandikishwaji wa anwani za makazi na Postikodi linaloendelea kitaifa.
Akizungumza mara baada ya kusomewa taarifa ya Mkoa na Mtehama wa Mkoa huo Yahya Madenge katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa amesema iko katika asilimia 97.
Nauye amefanya ziara Mkoani humo ya siku moja na kujionea utekelezwaji wa kasi na kueleza umuhimu wa anwani za makazi kuwa zoezi hilo litaleta manufaa katika Taifa kwa kuitambulisha Ramani ya Tanzania Kimataifa.
“Serikali imeona umuhimu wa kufanya zoezi hilo kwaajili ya kuitangaza inchi ya Tanzania pamoja na kurahisisha mawasiliano kwa mataifa mbali mbali”.
Hata hivyo Nauye ametoa wito kwa uongozi wa Mkoa na wananchi kuwa zoezi hilo litumike kuifadhi historia ya Mkoa huo na Taifa kwa ujumla ikiwemo vizazi vijavyo ziweze kujua historia kupitia majina ya mitaa na Barabara.
Mkuu Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amesema namna Mkoa wa Ruvuma unavyotekeleza zoezi la anwani za makazi na kufikia asilimia 97 na kushika nafasi ya 10 Kitaifa.
Ibuge amesema katika kuendesha zoezi hilo la anuani za Makazi Katika Halmashauri linatarajia kuisha April 15 na kuwasilisha taarifa kwenyekanzidata na kuweka vibao pamoja na namba kwenye makazi na Kitaifa April 30.
Ibuge amewapongeza wananchi wa Mkoa huo kwa namna ambavyo wameona ushirikiano kwa kupendekeza majina ya Mitaa yakiwemo ya Viongozi na kujitoa kugharamia pale panapohitaji gharama na kuongeza nguvu kwa kuhakikisha zoezi linakwenda vizuri.
Hizi nguzo tunazoziweka ni zoezi litakalokuwa endelevu, ndugu wananchi wa Mkoa wa Ruvuma zikalindwe tutoke kwenye ujima na ushamba wa nguzo kwa “sababu ni chuma na kuona chuma chakavu hiyo nayo ni kipimo kingine ambacho tutakuwa tumejishusha”
Imeandaliwa na Aneth Ndonde pamoja Jackson Mbano
Kutoka Kitengo Cha Habari na Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
April 13,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.